Menu
 

Na Mary Mosha,
Moshi.

WIMBI la matukio ya wanawake kujifungua na kuwatelekeza watoto limekuwa likiongezeka nchini ambapo katika tukio la kusikitisha  jeshi I la polisi mkoani Kilimanjaro,  limemuokota   kichanga kinacho dhaniwa kuwa ni cha siku moja  kikiwa kimetelekezwa   kando kando ya barabara  ya kibosho , wilaya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro.

Akidhibitisha ukweli wa tukio hilo, kamanda  mwandamizi wa jeshi la polisi la mkoani  wa Kilimanjaro Robert  Boaz ,  alisema, majira ya asubuhi ya jana, walipata taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna kichanga kimettelekezwa katika barabara ya kibosho.

Kamanda Boaz, alisema kichanga hicho chenye jinsia ya kiume, kinakadiriwa kuwa ni cha siku moja, vijana wake walifika maeneo hayo na kumchukua na kumkimbiza  katika hospitali ya rufaa ya  KCMC kwa ajili ya uangalizi wa madaktari wakati uchunguzi wa tukio hilo likiendelea.

“Tulimkuta mtoto huyo katika hali nzuri tu na kwa usalama zaidi, tumempeleka katika hospitali ya KCMC, chini ya uangalizi wa madaktari bingwa wa watoto,” alisema Boaz na kuongeza  kuwa

“ Askari wangu kwa sasa wanafanya uchunguzi ili kuweza kubaini ni nani aliyefanya kitendo hicho cha kinyama na tutakapofanikiwa kumkata hatua za kisheria zitachaukua mkondo wake,” alisema kamanda Boaz.

Kamanda boaz, alitoa wito kwa  wakazi wa maeneo hayo, kutoa taarifa ya mtu yeyote, aliyekuwa mjamzito awali na kwa sasa haupo kwa hali za kutatanisha, kutoa taarifa katika jeshi la polisi ili kuweza kumbaini mama wa mtoto huyo.
 

Post a Comment

 
Top