Menu
 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abas Kandoro akihimiza jambo wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake 
******
Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema mkoa wa Mbeya ambao ni watatu kitaifa kwa kuwa na asilimia kubwa ya maambuzi ya virusi vya Ukimwi (VVU) unahitaji mafunzo zaidi ili kuepusha maambuzi mapya ya ugonjwa huo.

Kandoro ameyasema hayo wakati akifungua kongamano la UKIMWI lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe tawi la Mbeya na kushirikisha wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu vilivyopo mkoani hapa.

Amesema Mkoa wa Mbeya una maambukizi makubwa ya VVU ambayo yanafikia asilimia 9.2 kiwango ambacho ni kikubwa kulinganisha na wastani wa maambukizi ya VVU kitaifa ambayo ni 5.7.

Amesema wakazi wa Mkoa wa Mbeya wanahitaji elimu zaidi ya maambukizi ya VVU ili kupunguza asilimia hiyo na pia kuwaepusha kupata maambuzi mapya kutokana na mkoa huo kuwa na majirani ambao wana asilimia kubwa zaidi ya maambuzi ya ugonjwa huo.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho, Dk Ernest Kihanga amesema kuwa Uongozi wa Chuo kwa kushirikiana na Serikali ya wanafunzi wameanzisha sera ya kupambana na ukimwi ili kuwakinga wanafunzi wasipate maambuki mapya ya VVU wawapo chuoni hapo.

Post a Comment

oversætte said... 21 June 2012 at 00:50

This must be Africaans?

Anonymous said... 22 June 2013 at 04:10

Ukimwi bado ni tatizo hasa kwa wanandoa.

Nzowa Godat said... 22 June 2013 at 04:18

Mbeya siku hizi hasa maeneo ya vijijini ngono uzembe imetawala.

 
Top