Menu
 

 Miili ya Marehemu ikiwa tayari imewasili katika Hospitali ya Rufaa Mbeya.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga, Mbeya.
Maiti 10 kati ya 13 zimetambuliwa na ndugu,kufuatia ajali iliyotokea juzi Juni 5 mwaka huu Mkoani Mbeya ikihusisha gari la abiria aina ya Coaster lenye nambari T 886 na gari ya mizigo aina Lori lenye kichwa nambari T 658 ASJ na tela nambari T 150 BDZ.

Mkuu wa usalama wa barabarani Bi. Butusyo Mwambelo, amewataja marehemu hayo kuwa ni Emmanuel Mwanjala mkazi wa Ilomba na Uyole jiji la Mbeya,Mwanike Focus mkazi wa Chunya na Uyole jijini hapa,Lucia Lingson(51) mkazi wa Katumba Wilaya ya Rungwe na Lena Ngomano(49) mkazi wa Ngumbulu Isongole Wilaya ya Rungwe.

Wengine ni pamoja na Pius Mbeya mkazi wa Uyole,Mwase Pius makazi wa Iganzo jijini hapa,Bahati Japhari(33) mkazi wa Kyela,Ernesta Kikanga(62) mkazi wa Ifunda Iringa, Dereva wa Coaster Mwasa Daimon(40) na Yerusalem Mwakyusa(35) wote ni wakazi wa Mbeya.

Bi. Mwambelo amesema kuwa maiti tatu bado hazijaweza kutambuliwa  na amewataka ndugu,jamaa na marafiki ambao ndugu zao hawajaonekana kufika katika Hospitali ya Rufaa kwa utambuzi wa maiti hizo.

Hata hivyo ameongeza kuwa dereva wa lori aliyesababisha ajali bado hajapatikana na juhudi za kumtafuta bado zinaendelea.

Post a Comment

 
Top