Menu
 

TUKO WANGAPI? TULIZANA.
MADA:-"Je,ni jambo la kawaida kabisa kwa wanaume au wanawake kuwa na zaidi ya mpenzi mmoja? Kwanini?".
Mtangazaji:- Greyson Salufu Chatanda a.k.a Chris Bee
Muda:- Saa 4:00 usiku mpaka 7:00 usiku.
Kipindi:- Bomba Special Show
Kituo:- Bomba FM Redio 104.0Mhz
Mahali:- Mbeya Tanzania.
<<<Bofya hapa kusikiliza live Bomba FM Radio>>>  
 MAONI YA WADAU.
Tuanze kwanza “tupo wangapi?” ni swali jepesi sana kwa kuliangalia lakini pia ni swali gumu sana kulijibu hata kwa wewe ndugu mtangazaji maana umesha pata jibu umewapanga wangapi hapo. Any ways suala la kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja inategemeana na mtu, kwanza kuna wanaume ambao ni tamani tamani yani wakiona dada mrembo wanakuwa na hamu ya kuwa nae kwa njia moja ama nyengine sio kwa kupenda bali tamaa tu ya ngono. Pia akina dada ndio usiseme wamekuwa na katabia kachafu sana hasa humu kwenye mitandao yetu ya jamii nazungumzia Facebook na mengineyo wakina dada hawa wakiona mtu ana marafiki wengi ama akiona profile ya mtu hata kama ni anafanyia kampuni feki basi watababaika na mwisho kuomba urafiki wakizani huyo ama hao watu ni wema kumbe ni nyoka tamaa nao zinawaponza na kutoka nje ya mahusiano na wapenzi wao. Mwisho kabisa naomba kibao cha
Profesa J msinitenge ama alikufa kwa Ngoma chake mwana fa na Komando Jide mimi Jembe la ukweli.

Frank Sigalla kutoka Ilemi jijini Mbeya sidhani kama ni kitu kizuri twaweza ambukizwa magonjwa.naomba nipigie wimbo wa Nako 2 Nako - Mchizi wangu remix iwaendee rafiki zangu wote pande hizi,bila kumsahau Efraim Luhanga ukipenda mwite Efrachemical wanaopenda chati nami 0756 25 59 75.

  Joshua Turuka Ni jambo la kawaida, sababu kubwa hakuna uamininifu,huenda kupitia mke/mme 1 kuna wasiwasi wa kuwa wengine zaidi ya wa3.

Hassan Othman true hiyo!sababu wazur wengi.

Hussein Rashid ni jambo la kawaida sana hususani kwa jamii ya kibongo, kwa sababu siku hizi hakuna mapenzi ya kweli, mtu anakupenda kutokana na ulichonacho mfukoni, ukiwa mtupu basi utaambulia kula vibovu.

Michael Tuingilege Me naona ni kawaida tu kama alidhishwi anatafuta mtu au anitafute MEME NIMPE UJoto 0715163933 mabint ambao awalidhishwi tu.play miss indepence ya neyo goesout to emmanuel james nyambo,abdul mbuyu playboyprezdent,joshua toruka,punch after punch

Luka Mbogela Kaka hiyo mi nadhani ni njaa ya starehe na ndio maana tunaita eti ni kawaida kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja

Alice Kunbert ni kawaida tu akili mukichwa..nitafurahi saaaaaana leo ukipiga kitu cha Senzo nyimbo ya I’ll be there maalumu kw marasta wt tz.nawapenda ile mbaya.

Lùdä Gängstèr Hiyo inatokana na ulimbukeni wa mapenzi. Ni Luda gangster kutoka DSM

  Brenda Tesha Wa Kwata Unity Arusha, ni jambo la kawaida kabisa ila sio vizuri pia kwani Mungu hapendi. Wengi wa wale wanaofanya hivyo ni kwa sababu wanadhani kuwa yule aliye nae akimsumbua kwa lolote wa ziada atamfariji.

Racquel Descheneles Ni ushamba tu na tamaa zao zinawasumbua, kwani hakuna kigeni!

Kutoka Italy ebwana inakuaje Bomba FM Radio. Mimi naona hili swala la kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja sio swala zuri na halileti faida yeyote dhidi ya kujihatarishia maisha. Na unachoweza kukivuna hapo ni kuweza kupata maradhi usiyoyategemea. Na chanzo cha yote haya husababishwa na tamaa, Hivyo napenda kuwashauri wale ambao wapo kwenye uhusiano basi waweze kuwa waaminifu kwasababu kama kweli unampenda ni kwanini usimlinde. Big up kwa Joshua Turuka, Scola Ledy, Yohana Shombe, Emmanuel James Nyambo pamoja na Maiko Jacob.

‎>niaje chris bee kwa hewa,,kuhusu mada nikweli wanawake kwa wanaume siku hizi ni fashion kuwa na wapenzi wengi,kwa mi naona chanzo ni tamaa za muda mfupi na matamanio ya kimwili tu,japo baadhi ya wanaume wanaona kama ni ufahari naurijali lakini sio hivyo kwani mwisho wa siku nikuishia katika maradhi kama UKIMWI nani kinyume na amri za Mungu,mpenzi mmoja tu anatosha,na ndie anaefaa kuwa mume au mke bora na sio wapenzi wengi,ni hayo tu,kutoka westzone shede kigoma,pamoja sana mzazi!

Mamujariath Hashim Sio jambo la kawaida mi nafikiri ni tamaa za kimwili pamoja na pesa ndizo zinapelekea mtu kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja

Boniface David Mwamwembe Ni kawaida tu,hiyo ni sababu ya kutokuridhika na ulichonacho.mi shada a.k.a maintainer toka ccm,nigongee k2 cha samicho

George Ng'umbi kama tulivyo kuwa na tamaa ya pesa ndivyo tulivyo hata kwenye mapenzi cause leo utamuona mzuri kesho utamuona mzuri zaidi yake by sam valentine
Patrick Benjamin Kuwana mpenzi zaidi ya mmoja ni kawaida hiyo hutokana maamuzi ya mtu hivyo basi wana takiwa kuwa makini sana na ukimwi.
Itibary Mohamed Jambo hilo kwa sasa limezoeleka kama ni la kawaida kwa sababu watu wengi wanaona kama ufahari fulani hivi ni kama kubadilisha mavazi Mbalizi ndio penyewe nipo pamoja sana.

Yohana Shombe kaka mi naona ni jambo la kawaida lakini kwa sasa mi naona ni ulimbukeni mtu kuwa na wapenzi wengi,kwani saizi magonjwa ni mengi.kama vipi chapisha ngoma ya Faddad nimeupata vipi special kwa michael minja,mark mush,brenda tesha,joshua turuka,fredy tony na rahimu yusuph,

Beatrice Vedastuce Vp?sababu ni tamaa za mwili na mali kwa wengine,kutokuridhika na wenzi wao.

Post a Comment

 
Top