Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Chunya.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mlimanjiwa na mkazi wa Kijiji cha Mlimanjiwa,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya Mussa Manyesa(9),amefariki dunia baada ya kutumbukia katika shimo la maji katika mgodi unaomilikiwa na Mrs Kasaka wa wilaya hiyo na kusimamiwa na Bwana Isaack Msowoya.

Tukio hilo limetokea Juni 16 majira ya saa 10 jioni,wakati mtoto huyo akiwa na wenzake na alipopita kando kando ya shimo hilo alitumbukia na kupoteza maisha papo hapo.

Baba wa mzazi wa marehemu Bwana Leonard Manyesa,amesema wakati wa tukio hilo alikuwa nyumbani kwake na muda mfupi alipata taarifa za mwanae kufariki,hali iliyompelekea kufika eneo la tukio,kisha kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa kijiji Bwana Shaban Masa.

Polisi walifika eneo la tukio na kuthibitisha kifo hicho na kuwaruhusu ndugu wa marehemu kuuchukua mwili wa marehemu na mazishi ya kuuaga mwili huo yalifanyika Juni 17 mwaka huu  kijijini hapo.

Wakati huo huo,katika Kijiji cha Ikandana,Wilaya ya Ileje mkoani hapa Mzee Obadia Mtafya mwenye umri kati ya miaka 80-85,amefariki dunia baada ya kujinyonga kwa kutumia shuka chumani kwake.

Aidah,hakuna sababu zilizotolewa kuhusiana na kifo chake,tukio ambalo limetokea majira ya saa nne usiku na wakati wa tukio ndugu hawakuwepo nyumbani hapo.

Jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na kwamba mazishi ya Mzee Mtafya yatafanyika Juni 19 mwaka huu kijijini hapo.

Post a Comment

 
Top