Menu
 

 Taa za barabarani Jijini Mbeya.
*******
Habari na Angelica Sullusi, Mbeya.
Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya,Bwana Juma Idd amesema mradi wa kuweka taa za barabarani kuanzia Stendi Kuu ya mabasi hadi Uyole umeshaanza kutekelezwa ingawa taa hizo hazijaanza kuwaka kutokana na ukosefu wa mita za umeme.
 
Amesema katika barabara Kuu za Stendi -Meta na ile ya Tanzam kuanzia Meta hadi Uyole, taa za barabarani tayari zimesimikwa hadi eneo la Sae na kuwa taa hizo zinasubiri mita za umeme kutoka Tanesco ili zianze kuwaka.
 
Amesema ikiwa hata leo zitapatikana angalau mita mbili za umeme, taa za barabarani kuanzia Stendi Kuu hadi Meta zitaanza kuwaka mara moja na zile za kuanzia Meta hadi Sae zitasubiri miundombinu kikamilike.
 
Aidha,amesema mradi huo pia unahusisha uwekaji wa taa kwenye kituo cha mabasi madogo maarufu kwa jina la daladala cha Kabwe ambacho pia kazi ya kusimika nguzo za taa na kufunga taa tayari imekamilika.
 
Idd amesema kuwa mradi huo unatekelezwa kwa ubia baina ya Halmashauri ya Jiji na kampuni ya Sika Angence ambayo ndiyo yenye wajibu wa kujenga miundombinu ya taa hizo pamoja na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom ambayo imechukua nafasi ya kuweka matangazo yake kwenye nguzo hizo.

Post a Comment

 
Top