Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Wimbi la wananchi kujimilikisha silaha Wilaya ya Chunya,Mkoani Mbeya limeendelea tena baada ya mkazi mwingine wa wilaya hiyo kukamatwa akimiliki silaha kinyume cha sheria.

Bwana Felix Chombe(38) mkulima na mkazi wa Gua wilayani humo amekamatwa nyumbani kwake majira ya saa nne asubuhi Juni 14 mwaka huu,akiwa na silaha aina ya gobole.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa Diwani Athuman amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi lake pindi upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.

Hata hivyo ameongeza kuwa mtuhumiwa Bwana Shombe pia ni mwindaji haramu.

Post a Comment

 
Top