Menu
 Chifu wa kijiji, Chinamhora, aliyetoa tamko la kukamatwa watu hao.
KATIKA tukio la aina yake, mwanaume mmoja na mama yake mzazi wamekuwa na uhusiano wa kimapenzi ambao umesababisha mwanamke huyo kupata mimba mara mbili. Simon Matsvara na Ethel Vhangare ni wakazi wa kijiji cha Pote.

Simon alimpa ujauzito mama yake wakati baba yake, Agripah Matsvara, alipokuwa hai, na akampa ujauzito mara ya pili baada ya kifo chake.

Mara ya kwaza ujauzito huo ulitoka, lakini wakati huu Vhangare anadaiwa kuwa na ujauzito wa miezi mitano alioupata kutoka kwa Simon.

Watu hao wanasemekana kuwa wamekimbia baada ya msako wa kuwakamata ulioamrishwa na Chifu.

Inasemekana mwaka 2008, Agripah, alipatwa na kiharusi ambapo wawili hao walisaidiana kumuuguza, lakini baadaye mama huyo akaanza kuwa anatapika na kuwaeleza majirani kwamba alikuwa mjamzito na mhusika ni mwanaye.

Wanafamilia wanasemekana waliwapiga faini kwa kuwaambia watoe n'gombe ambao idadi yake haikufahamika.

Hata hivyo, mwaka huo wa 2008, mimba ya Vhangare iliharibika kabla ya mumewe kufariki mwaka huohuo. Hata hivyo, Simon na mama yake waliendeleza uhusiano wao wa kimapenzi na mama huyo kupata mimba tena ambapo amri ya kuwakamata ilitolewa ili kuwaadhibu kwa kitendo hicho cha aibu.

Post a Comment

 
Top