Menu
 

*Afisa mtendaji wa Kata akaa kwenye kituo zaidi ya miaka 20.
*Afisa Mtendaji wa Kijiji naye ajimegea shilingi 380,000.

Mkataba wa ahadi ya kulipa fedha kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Masanyila,anaedaiwa kufuja pesa taslimu shilingi 2,350,000 za zahanati ya kijiji.
******
Habari kamili na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
 Mwenyekiti wa Kijiji cha Masanyila,Kata ya Igamba,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Bwana Chepson Mkanjilwa,anatuhumiwa kuiba pesa taslimu 2,350,000,kati ya shilingi milioni 12 zilizotolewa na Halmshauri ya Mbozi kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kijiji hicho iliyogharimu zaisi ya miliozi 24 lakini mpaka sasa haija kamilika.

Katika katika mkutano uliofanyiaka Julai 21 mwaka 2011 mwenyekiti huyo,alikirikutumia pesa hizo kwa matumizi yake binafsi na alipobanwa siku hiyo alitoa shilingi laki mbili na salio la 2,150,000 kuahidi mbele ya mkutano huo wa hadhara kwa uthibitisho wa kuweka saini kwenye barua ya mkataba mbele ya Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Justin Mgala lakini hajazirejesha.

Kufuatia hatua hiyo Wenyeviti wa vitongoji 6 vya Kijiji hicho walikutana na kumwalika Diwani wa Kata hiyo mheshimiwa Amos Kalonge,lakini hali ilikuwa ndivyo sivyo kutokana na mwenyekiti na afisa mtendaji wa kijiji kuingia mitini.

Katika hali hiyo isiyokuwa ya kawaida Afisa mtendaji Bwana Mgala,anatuhumiwa kwa kufuja shilingi 380,000 alizokabidhiwa na Mkandarasi kwa ajili ya kununulia mchanga wa kujengea nyumba ya Daktari wa zahanati ya kijiji na mpaka sasa haonekani ofisini kwake,licha ya kupewa uhamisho kwenda kijiji kingine huku wananchi wakiwa hawajui la kufanya.

Kwa upande wake Mheshimiwa Kalonge,aliwataka viongozi hao na wananchi kuahirisha mkutano huo hadi Juni 27 mwaka huu na atamuomba Mkurugenzi wa Halmashauri na Mkuu wa Wilaya ili waweze kusikiliza kero za wananchi wa kijiji hicho.

Aidha,wananchi hao wamemtupia lawama Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bwana Ambakisye Waya,,ambaye amedumu katika kata hiyo kwa takribani miaka 20 sasa na kudai kuwa amekifanya kijiji kama mradi wake wa kufuja fedha kupitia watendaji wa vijiji na akishatimiza azma yake huwahamisha watendaji hao vituo vya kazi hali inayopelekeza pesa za wananchi kupotea ovyo.

Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi Bwana Levson Chilewa,amekiri kupokea malalamiko ya kijiji hicho na kwamba ofisi yake ilituma mkaguzi hivyo taarifa yake ataitoa siku za hivi karibuni.

Post a Comment

 
Top