Menu
 

Team Tanzania baada ya kumaliza matembezi ya Susan G.Komen. dhidi ya kupiga vita maradhi ya Saratani ya maziwa. (Picha maelezo na swahilivilla.blogspot.com)

Team Tanzania iliochangamsha katika matembezi ya 2012 Susan G. Komen Global Race for  Care.
Mamia ya wananchi kutoka majimbo mbalimbali nchini Marekani wakiwemo Team Tanzania waliojitokeza kwa wingi kwenye matembezi na mbio za 2012 Susan G. Komen Global Race for  Care ya kumaliza vita dhidi ya maradhi ya Saratani ya Maziwa  hapa jijini Washington DC Nchini Marekani.

Ni mfano mzuri wa kuikwa nchini Tanzania kama kujali na kuwapa moyo kina mama walioathirika na saratani ya maziwa kwani pia wanahitaji kutaminiwa, kutoa elimu ya kujikinga pamoja na wale walioathirika na ugonjwa huo, ili kupata changamoto za kwenda kupima kila mwenzi, kwani ni ugonjwa hatari unao waumiza  sana kina Mama wa Mijini na Vijijini huko nyumbani.

Tungeliomba makampuni  makubwa kufikiria zaidi na kuwasiliana na Uongozi Mzima wa Team Tanzania ambao wana uzowefu mkubwa katika Susan G. Komen Global Race for  Care, wanaweza kukupeni mawazo zaidi juu ya  kutoa msaada huo kwa kina mama walioathirika na wale familia zao tayari wameshakubwa na ugonjwa huo  wa Saratani ya Maziwa.

Ili kutoa mifano kwa wengine ambao bado wanahitaji mafundisho ya kujikinga na ungojwa huo, kwa mwendo huo wa mkosanyiko wa watu ambao utaleta muamko mkubwa na elimu  kwa waTanzania wote, na kujisikia tupo katika muamko flani dhidi ya kutokomeza ugonjwa huu hatari unao wakumba kina Mama wote Duniani.


Vile vile Team Tanzania imetoa shukurani kwa waTanzania wote  walioshiriki katika matembezi ya "Susan G. Komen Global Race for the Cure", pamoja na wale ambao hawakuweza kushirikiana nao kwa michango yao mbali mbali katika kufanikisha shughuli hii.

Pia walitoa shukurani kubwa kwa Ubalozi wa Tanzania Nchini Marekani, kwa ushirikiano wao waliotoa kuweza kufanikisha shughuli hiyo, pia kutoa shukurani kwa vyombo vya mawasiliano katika Jumuia ya Watanzania kwa mchango wao mkubwa wa kutawanya habari hizo.

Nimifano mzuri wa kuikwa, na niwajibu wetu kufikisha habari hizi nyumbani ili iwe kama zawadi ya mafundisho ya kile tulichokichuma ugenini kukileta nyumbani, ili waathirika wa ugonjwa huu hatari tuweze kuutokomeza kwa hali na mali, kuwa kitu kimoja kama waTanzania tunaojali na kuthamini nchi yetu, kwani kitaifa tunaweza.

Angalia kwa makini Video ya mamia ya wananchi waliojitokeza kwa wingi kwenye mbio za Susan G.Komen. kumaliza vita dhidi ya maradhi ya Saratani ya Maziwa Susan G.Komen. 2012!Post a Comment

 
Top