Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Half London,inayomilikiwa na Bwana Raphael Mwasongole,mkazi wa Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya imeteketea kwa moto.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku Juni 28 mwaka huu na kusababisha moto mkubwa ulioteketeza vyumba zaidi ya 20 na kila kitu kilichokuwemo ndani yakiwemo magodoro na samani huku watu walikuwemo wamelala kunusurika kifo,baada ya kuvunja milango na madirisha na kubeba mizigo yao.

Kwa mujibu wa mmiliki wa nyumba hiyo Bwana Mwasongole,amesema ameshindwa kumudu kuuzima moto huo kutokana na uhaba wa maji na gari ya Zimamoto wilayani humo,ambapo moto huo uliendelea mpaka majira ya saa 12 asubuhi.

Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa chanzo cha moto huo ni mshumaa,uliowaka katika moja ya vyumba na kuendelea katika vyumba vingine.

Wameongeza kuwa umeme katika nyumba hiyo haukuwepo kutokana na Luku kuisha,hali iliyopelekea kuwashwa kwa mishumaa katika vyumba.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mbeya Diwani Athuman,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi unaendelea na pia thamani ya vyombo vilivyoteketea haijajulikana.

Post a Comment

 
Top