Menu
 

Mshindi nambari moja Winfrida Paulo(katikati) akifuatiwa na mshindi wa pili Sabrina Abdul(kulia) na Mshindi nambari tatu Careen Elias(Kushoto),katika Mashindano ya Miss Redds Mbeya 2012,ambapo Warembo 12 kutoka wilaya zote za mkoa wa Mbeya walishindani taji hilo. Tukio lililoandaliwa na Kituo cha Redio Bomba FM 104.0Mhz Mbeya na kudhaminiwa na Kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redds, SBC Tanzania LTD kupitia kinywaji cha Mountain Dew, Masasi Fashion, Access Computer LTD, Beaco Resort, Grace College, Shaba Pub na Mfikemo Hotel na litasindikizwa na burudani toka kundi la Coast Modern Taarab a.k.a Watafiti wa mipasho.
 Mshindi wa Taji la Miss Redds Mbeya 2012 Winfrida Paulo aliyekati muda mfupi baada ya kuvishwa taji hilo na aliyekuwa Miss Mbeya 2011(bluu), katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Jijini Mbeya na kusindikizwa na Burudani kutoka Kundi nzima la Mambo ya Mwambao Coast Modern Taarab kutoka Jijini Dar es Salaam.
Pichani aliyekuwa Miss Mbeya 2011(gauni la bluu), akimvisha taji alilotwaa mwaka jana Mshindi wa Miss Redds Mbeya 2012 Winfrida Paulo.
 Washindi wa nafasi ya 1,2 na 3 wa Miss Mbeya 2011 wakiwa katika picha ya pamoja muda mfupi kabla ya kukabidhi mataji hayo kwa washindi wa Miss Redds Mbeya 2012.
Warembo walioingia katika Tano bora ya washiriki wa shindano la Miss Redds Mbeya 2012, ambpo jumla ya warembo 12 kutoka wilaya za jiji warembo 5, Mbeya vijijini warembo 3 , Mbalali 1, Chunya 1 na Mbozi mshiriki 1 walipanda katika jukwaa moja.
 Wasanii wa Kundi la Coast Modern Taarab a.k.a Watafiti wa Mipasho akiwemo Kibibi Yahaya(Kulia),Mauwa Tego(wa pili kutoka kulia), wakitoa burudani katika shindano la Miss Redds Mbeya 2012, lililoudhuriwa na wakazi wengi wa Mkoa wa Mbeya.
  Wasanii na wapiga vyombo wa Kundi la Coast Modern Taarab a.k.a Watafiti wa Mipasho akiwemo Omary Tego(aliyevalia suti rangi bya maziwa) wakiwa katika picha ya pamoja kablya ya kutoa burudani katika shindano la Miss Redds Mbeya 2012, lililoudhuriwa na wakazi wengi wa Mkoa wa Mbeya.
 Mgeni rasmi katika Shindano la Miss Redds Mbeya 2012 Bwana Geofrey Anania,ambaye pia ni Katibu tawala wa Wilaya ya Mbeya akizungumza wakati wa shindano hilo.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Adili(kulia),ambaye pia ni Mkurugenzi wa Chapakazi Production iliyopo jijini Mbeya.

*****Usikose kutembelea kesho kupata mwendelezo wa matukio mbalimbali ya shindano hili*****

Post a Comment

 
Top