Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Treni ya mizigo yenye namba MB inayomilikiwa na mamlaka ya reli nchi zaTanzania na Zambia(TAZARA) imeacha njia na kusababisha behewa moja kupinduka.

Ajali hiyo imetokea umbali wa Kilometa 861 kutoka Dar es salaam katika eneo la Mbeya na Mbalizi,treni hiyo ikiendeshwa na madereva Chanda Malukusha na Atinui Phiri

Mnamo Juni 13 mwaka huu majira ya saa saba na dakika arobaini treni hiyo iliacha njia na kusababisha kupinduka kwa behewa moja lenye nambari 2018.

Treni hiyo ilikuwa ikitokea nchi ya Zambia kuelekea jijini Dar es salaamTanzania,ambapo haikuleta madhara kwa binadamu yeyote wala mali.

Hata hivyo chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman na amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Post a Comment

 
Top