Menu
 

Habari na Tumaini Msowoya,Iringa.
Wataalamu wa wizara ya afya na ustawi wa jamii wameishauri serikali kubuni njia mpya ya ufadhili wa masomo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini ili kuepusha mitandano ya kingono inayoendelea kuiathiri jamii ya wasomi ambayo inateketea kwa ugonjwa wa ukimwi kutokana na kukabiliwa na hali ngumu ya maisha vyuoni.

Afisa Ustawi wa Jamii wa Wizara ya Afya, Eliwanzita Mtebe amesema katika vyuo vya elimu ya juu vilivyopo hapa nchini, idadi kubwa ya wanachuo katika vyuo hivyo wanaambukizwa virusi vya ukimwi na kupoteza maisha ume vingi.

Mtebe alikuwa akizungumza katika warsha ya siku moja kuhusu kampeni ya kitaifa dhidi ya mitandao ya kingono maarufu kama ‘Tuko Wangapi’ iliyowahusisha Waandishi wa Habari wa mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya.

“Mitandao ya ngono huko katika vyuo vikuu ni balaa na nyie ni mashahidi kwamba wanapocheleweshewa mikopo hali huwa mbaya zaidi hasa tunapowaona dada zetu wanavyojiuza kirahisi kwa sababu hawana fedha,wengine wakizidiwa wanaiba na ndipo mitandao hii ya kingono inapo sambaza VVU na kila wakati utaona wanachuo na walimu wao wanavyopoteza maisha,”alisema.

Alisisitiza kuwa  ipo haja kwa serikali kuangalia upya njia bora za utoaji wa mikopo tofauti na ilivyo hivi sasa.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Iringa,Bi. Getrude Mpaka aliwataka wanandoa na watu walio katika mahusiano kwa waaminifu katika mahusiano yao ili kupunguza mitandao ambayo imekuwa ikihatarisha afya zao kutokana na mambuziki ya Ukimwi.

Alisema mitandao ya kingono  imekuwa ikiathiri Serikali baada ya  tafiti za Wizara ya Afya na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kuonyesha kuwa ya hali hiyo yanasababisha mifarakano katika familia na kuziathiri kisaikolojia, kiafya, kielimu na hata kuendelea kuathiri jamii kwa ujumla.

Awali, Mganga Mkuu wa mkoa wa Iringa,Dk.Robert Mahimbo alisema kuwa asilimia 20.7 ya wanaume wote nchini na asilimia 3.5 ya wanawake kwa mujibu wa TACAIDS,tafiti zinaonyesha kwamba wana mahusiano ya kingono kwa zaidi ya watu wawili.

Post a Comment

 
Top