Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia watu watano katika matukio manne ya kukutwa na pombe aina ya moshi(gongo) na mwingine kukutwa na kete za bangi.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Diwani Athumani,amesema waliokamatwa na pombe hiyo haramu ni pamoja na Amani Mwaikambo(35),mkazi wa Kijiji cha Ilenge,Kata ya Kiwira ambaye alikamatwa Juni 12 mwaka huu majira ya 11 jioni akiwa na pombe hiyo lita 9.

Mwingine ni Dorethea Adamson(30),mkazi wa Tandale alikamatwa saa 9:47 alasiri akiwa na lita 4 za gongo na majira ya 9:45 jioni Polisi wakiwa katika doria walimkamata Boniface Mwakibete(54) mkulima na mkazi wa Ilongoloto alikamatwa akiwa na lita 5 za pombe hiyo haramu.

Kamanda Diwani amemtaja mtuhumiwa mwingine wa pombe hiyo Maria Paulo(33) mkulima na mkazi wa Kamficheni,Wilaya ya Chunya ambaye alikamatwa Juni 12,majira ya saa 3 usiku akiwa na gongo lita 5.

Ameongeza kuwa watuhumiwa wote ni wauzaji wa pombe hiyo haramu(gongo) ma kwamba upelelezi ukikamilika watafikishwa katika mahakama kusomewa mashtaka.

Hata hivyo Kamanda Diwani amesema Juni 12 majira ya saa 9:30 alasiri huko Kiwila Kati,Polisi walimkamata Lusako Aswile(21),ambaye alikamatwa na Kilo moja ya bangi.

Wakati huohuo watuhumiwa wote wapo mahabusu na taratibu za kuwafikisha mahakamani zinafanyikana upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.

Post a Comment

 
Top