Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watu wawili wameuawa Mkoani Mbeya na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi,Juni 14 mwaka huu majira ya saa saba usiku katika Kitongoji cha Maleza,Kijiji cha Kilyamatundu,Kata ya Kipeta Wilaya ya Sumbawanga Vijijini.

Afisa Mtendaji wa Kata husika Bwana Joseph January Ninde,amewataja marehemu kuwa ni pamoja na Isaack Sanga(53),ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Mbeya na Paulo Chambanenje(35),mkazi wa Maleza,Kata ya Kamsamba Wilaya ya Momba mkoani hapa.

Katika tukio hilo mwanamke mmoja alijeruhiwa vibaya kwa risasi,ambaye alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa iliyopo jijini Mbeya.

Bwana Ninde,amesema watu hao waliodhaniwa kuwa ni majambazi walifika katika kijiji hicho na kuwavamia watu hao,waliofika kijiji hapo kununua zao la mpunga majira ya saa saba usiku na kufyatuliwa risasi,kisha kuwapora pesa taslimu shilingi 5,400,000 ambazo walitoroka nazo kusikojulikana.

Miili ya marehemu imesafirishwa kutoka eneo la tukio na kupelekwa kwenye makazi yao,ambapo mwili wa marehemu Sanga umesafirishwa kwenda Mbeya na Chambanenje kwenda Kijiji cha Maleza.

Kumekuwepo na tatizo la mawasiliano kijiografia kwani eneo la tukioni mpakani mwa mikoa ya Rukwa na Mbeya.

Hata hivyo baadhi ya wananchi wamedaiwa kuwa wahalifu wa matukio wanafahamika lakini jeshi la polisi halichukui hatua dhidi ya wahalifu hao.

Post a Comment

 
Top