Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Watu wawili wameuawa kwa tuhuma za wizi wa ng'ombe mmoja mali ya Bwana Rafael Sikanyika,Kijiji cha Malonji,Kata ya Ihanda,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya.

Marehemu hao wametambuliwa kwa majina ya Bonny Haonga(23) na Andovile Mwasalvuwa(16) wote ni wakazi wa Ihanda kwa pamoja wanatuhumiwa kuibakatika kijiji cha Malonji umbali wa kilometa 7 kutoka kijiji walichokuwa wakiishi.

Tukio hilo lilitokea Juni 13 mwaka huu limetokana na wananchi wenye hasira kupata taarifa za wizi wa ng'ombe huyo ambaye thamani yake haikufahamika,ambapo waliamua kumfuatilia na kuwakamata wezi hao eneo la Ihanda Relini na kisha kuwapiga na kuwateketeza kwa moto.

Afisa mtendaji wa Kata hiyo Bwana Amos Kyomo amesema alipata taarifa majira ya saa moja asubuhi,June 13 mwaka huu na kisha kufika eneo la tukio ambapo aliatoa taarifa Kituo cha Polisi Mbalizi ambao nao walifika na kuuchukua miili ya marehemu hadi Hospitali ya Wilaya ya Mbozi kwa ajili ya uchunguzi.

Aidha mara baada ya uchunguzi kufanyika miili hiyo ilikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika katika maeneo ya Ihanda jioni ya siku hiyo hiyo.

Hata hivyo Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa Diwani Athumani,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi lake linafanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo.

Matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi yamekithiri kwa siku za hivi karibuni Mkoani Mbeya,licha ya Polisi kuelimisha kupitia sera yake ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

Post a Comment

 
Top