Menu
 

Pichani ni Producer Baucha.
"Mambo vipi?......Nimefiwa na Baba mzazi leo usiku Julai 4 2012,najua wewe ni mtu muhimu kukutaarifu, Kwanza nasubiri kuelekea Zanzibar kwa mazishi.....Baucha

Kwa mujibu wa SMS yake aliyonitumia saa 9:30  usiku Ally Baucha ambaye ni mmiliki na producer wa studio za kurekodia muziki maarufu kwa jina la BAUCHA RECORDS na mara baada ya taarifa hizi nilifanikiwa kuzungumza naye pia usiku huu huu.

 Baucha amesema kifo cha baba yake Mzee Mohamed Yussuf kimetokana na ugonjwa wa ini na amefariki akiwa na umri wa miaka 69 na pia aliwahi kuwa mkuu wa polisi wa wanamaji mkoa wa Mwanza miaka ya 1980 kabla ya kuhamishiwa Zanzibar.


 Tuzidi kumwombea kwa Mola amtie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu
.....SOTE NJIA YETU NI MOJA.... MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU BABA YAKE ALLY BAUCHA .... AMEN

Post a Comment

 
Top