Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Chifu Merere II wa kabila la Wasangu,ameingia matatani tena baada ya kudaiwa kuchukua pesa kutoka kwa familia ya marehemu Frank aliyefariki juzi Julai 11 mwaka huu katika Kijiji cha Ijumbi,Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.

Chifu huyo alitakiwa kurejesha fedha zilizotumika katika tambiko ili marehemu huyo apone,lakini hali ikawa tofauti na kufariki,kufuatia tukio hilo wananchi waliandamana na kumtaka chifu huyo kurejesha pesa na kutishiwa kuzikwa akiwa hai.

Aidha Merere II alizilipa pesa hizo katika uongozi wa kata hiyo,pamoja na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha wilaya hiyo na baadae kuachiwa huru.

Hata hivyo jana Chifu Merere II aliifuata familia ya marehemu Frank na kuitaka kutoa shilingi 250,000,akidai fidia ya pesa hizo alizokuwa amezirejesha Julai 11 ndipo wananchi waligadhibika na kutaka kumkamata.

Wakati tukio hilo likiendelea Afisa Mtendaji wa kata hiyo Bwana Jordan Masweve akiwa na sungusungu walimuokoa Chifu huyo kutoka nyumbani kwake na ku,hifadhi katika ofisi ya kata,huku ulinzi mkali ukiwa umeimarishwa.

Post a Comment

 
Top