Menu
 

Chifu Merere II wa kabila la wasangu.
******
 Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Chifu Merere II (70) wa kabila la wasangu,amenusurika kuzikwa akiwa hai baada ya kutokea tafrani katika msiba wa kijana aliyefahamika kwa jina moja la Frank,katika Kijiji cha Ijumbi,Kata ya Ruiwa,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limefuatia baada ya chifu huyo akishirikiana na ndugu kukubali kwenda kupiga ramli ya ugonjwa wa kijana huyo baada ya kifo kwa Mganga wa kienyeji aishie Wilaya ya Mbozi,ambaye jina lake hakutajwa na mganga huyo kuagiza kuchinjwa ng'ombe mmoja na kupikwa pombe katika pipa lenye ujazo wa debe 12.

Kufuatia agizo hilo marehemu aliuza sehemu ya uwanja aliokuwa anaumiliki kwa zaidi ya shilingi 450,000 na Chifu Merere II kukabidhiwa pesa hizo kwa ajili ya tambiko.

Aidha baada ya makabidhiano hayo ng'ombe alichinjwa,pombe kupikwa na kuitwa baadhi ya wanandugu mwanzoni mwa mwezi Julai mwaka huu na kwamba baada ya tambiko marehemu atapona.Mganga huyo alidai waliomroga marehemu huyo ni ndugu wa karibu na majirani licha ya kutoweka wazi majina yao.

Sakata la Chifu Merere II kutaka kuzikwa akiwa hai limekuja baada ya marehemu Frank kufariki Julai 10 mwaka huu na vijana wa kijiji cha Ijumbi kutaka maelezo kwanini marehemu amefariki kutokana na sadaka kutolewa huku marehemu akiuza kila kitu alichokuwa nacho.

Aidha haikuishia hapo vijana hao waligoma kuchimba kaburi na kumtaka Chifu huyo atoe maelezo ya kwanini marehemu amefariki lasivyo arudishe pesa vinginevyo atazikwa akiwa hai ili iwefundisho.

Naye,Afisa Mtendaji wa Kata Bwana Jordan Masweve,alipopata taarifa hizo alienda nyumbani kwa Chifu na kukuta vijana wamemzonga wakimdai pesa zilizotumika katika tambiko.

Hata hivyo Chifu Merere II alikuwa hana la kujibu,ndipo Afisa mtendaji huyo alimchukua na kwenda kumfungia mahabusu na yeye kwenda msibani na kuitisha mkutano wa hadhara,ambapo aliwaomba wananchi wakachimbe kaburi huku yeye akiahidi kumfuatilia Chifu huyo ili arejeshe pesa hizo.

Pamoja na vijana hao kukubali kuzika majira ya saa 8 mchana,hali ilizidi kuwa tete ndipo Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Diwani Athuman alituma askari kijijini hapo kwa ajili ya kuimarisha amani na kumwokoa Chifu huyo baada ya mazungumzo marefu na baadhi ya pesa shilingi 350,000 kurejeshewa aliyenunua uwanja.

Wakati kiasi kilichobaki Diwani wa kata hiyo Mheshimiwa Alex Mdimilage amesema watafanya utaratibu wa kuzirudisha katika familia ya ndugu wa marehemu,na chifu Merere II kuachiwa majira ya saa 12 jioni na amani kurejea kijijini hapo.

Siku chache zilizopita mwanamke mmoja wa Kijiji cha Malamba,Kata hiyo Bi Rozina Mwadala(60),aliyezikwa akiwa hai Juni 2 mwaka huu baada ya kutuhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina baada ya Mganga wa kienyeji huyo huyo kutoka Wilaya ya Mbozi kupiga ramli kwa madai kuwa marehemu aliyezikwa hai ndiye aliyesababisha kifo cha mkazi mwingine wa kijiji hicho marehemu Frank Lingo(25),aliyefariki Juni Mosi mwaka huu kwa maumivu kwenye sikio na jicho.

Post a Comment

 
Top