Menu
 

Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Idadi ya washindi wa promosheni ya Vuna Mkwanja inayoendeshwa na Kampuni ya vinywaji baridi ya Cocacola tawi la Mbeya, imeendelea uongezeka mkoani Mbeya baada ya watu wawili kuzawadiwa shilingi milioni moja kila mmoja na mwingine shilingi laki moja walizojishindia baada ya kunywa soda za kampuni hiyo.

Washindi hao wamekabidhiwa fedha zao juzi kwenye kituo cha mabasi madogo maarufu kama daladala katika eneo la Sido mbele ya umati mkubwa wa watu waliojitokeza kushuhudia tukio hilo.

Nafed Sanga, makazi wa Tunduma wilayani Mbozi na Juma Aron Kaseka mkazi wa mji mdogo wa Mbalizi ndio walioibuka na kitita cha shilingi milioni moja kila mmoja .

Mwingine ni msichana Liliani Jubel ambaye ameambulia shilingi 100,000 baada ya kunywa soda ya Coca Cola kwenye eneo la tukio na kubahatika kushinda kiwango hicho cha fedha.

Wakizungumzia namna walivyofanikiwa kupata zawadi hizo washindi hao wamesema suala ni kunywa vinyaji vinavyozalishwa na kampuni ya coca cola.

Akikabidhi fedha hizo kwa washindi, Meneja Mauzo wa kampuni ya Coca Cola Nyanda za Juu Kusini, William Nguji amesema kuwa ni rahisi kwa mtu yeyote anayekunywa bidhaa za kampuni ya Coca Cola kuibuka mshindi kwani zawadi zilizotengwa kwa ajili ya promosheni hiyo ni nyingi.

Amesema katika promosheni hiyo kuna zawadi ya soda ya bure, fulana, kofia, fedha taslimu shilingi 2,000 na shilingi 10,000 ambazo washindi hukabidhiwa pale pale kwa muuzaji wa vinywaji vya kampuni ya Coca Cola.

Post a Comment

 
Top