Menu
 

 Na Sjomi Mtaki, Tunduma.

Jeshi la polisi mkoani Mbeya limefanikiwa kudhibiti maandamano makubwa ya baadhi ya wananchi yaliyokuwa yamepangwa kufanyika mjini hapa kinyume na sheria.
 
 Lengo la mpango huo ulikuwa ni kufikisha ujumbe kwa serikali ili iweze kukarabati au kujenga sehemu ya kipande cha barabara chenye urefu wa wa kilometa moja kinacho anzia maeneo ya Customs hadi kanisa la Roma katika barabara ya iendayo Sumbawanga.
 
 Tukio hilo lilitokea hivi karibuni majira ya alfajiri mjini hapa wakati kikosi cha polisi cha kuzuia fujo (FFFU}  kikiongozwa na kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya,kilisambazwa katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya mjini hapa.
 
 Askari hao ambao walitumia magari matatu aina ya Land Rover yenye namba za usajili TP 1465,TP 1466 na TP 2079 walikuwa wamevalia mavazi rasmi kwa ajili ya kukabiliana na jambo lolote la uvunjivu wa amani walionekana kuchukua tahadhari
 kukabiliana na hatua za uvunjifu wa amani kama ungetokea.
 
 Taarifa za awali zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio,zilidai kuwa pamoja na kuwepo mpango huo wa maandamano pia wananchi hao waliazimia kufunga barabara ya Tunduma unbawanga kwa muda usiojulikana ili kuzuia magari yasipite kwenda Mbeya na nchi jirani ya Zambia.
 
 Diwani wa kata ya Tunduma Franck Mwakajoka,alisema wananchi hao wanahaki ya kudai ujenzi wa barabara hiyo kwa kuwa sehemu hiyo ipo katika mpango wa ujenzi wa  mradi mkubwa wa ujenzi wa barabara ya Tunduma hadi Sumbawanga.
 
 Mwakajoka alisema inashangazwa kuona sehemu hiyo ya barabara haijaguswa na mkandarasi wa ujenzi,ambaye alinzia kujenga mbele ya eneo hilo na kuacha sehemu hiyo ambayo kwa sasa iko katika hali mbaya ikiwa na mashimo mengi.
 
 Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani,alisema kikosi hicho kilifika mjini humo baada ya kupata taarifa za uhakika kuhusiana na mwenendo mzima na athari ambazo zingeweza kujitokeza kwa raia na wafanyabiashara.
 
 Alisema taarifa hizo zilfikishwa na kujadiliwa katika kamati ya ulinzi na usalama chini ya mwenyekiti wake mkuu wa mkoa huo Mheshimiwa Abas Kandoro,ambaye alitoa magizo kwa meneja wa Tanroad mkoani mbeya kwenda eneo hilo ili kutoa majibu sahihi ya madai ya wananchi hao.
 
 ,”Ukweli mpango huo hakuwa halali na huenda ungesababisha usumbufu mkubwa kwa raia wasiokuwa na hatia,wasafiri wangepata usumbufu mkubwa na biashara zingesimama kufuatia hali hiyo bila shaka vurugu zingeweza kujitokeza,”alisema.
 
 Kwa upande wake meneja wa barabara nkoani Mbeya James Nyabakali alieleza “Uhuru”kuwa mdai ya wananchi hao yamepata ufumbuzi kwa kuwa sehemu hiyo ya barabara itaanza kufanyiwa ukarabati baada ya miezi miwili ijayo.
 
 kuunganisha ujenzi wa sehemu ya barabara hiyo itafuatwa baada ya serikali kufanya upembuzi yakinifu kwa kuwa katika eneo hilo kuna mali za watu.
 
 Mji wa Tunduma umekuwa kinara  kwa kuwa na maandamano ya mara kwa mara ambayo baadhi yake imekuwa ikileta athari kubwa kwa upande wa jamii,hivyo kuleta tishio kwa baadhi ya wafanyabiashara kuuimbia mji huo.

Post a Comment

 
Top