Menu
 

Na Bosco Nyambege,Mbeya
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linawashikilia vijana wawili kwa tuhuma za kukutwa kete za bangi gramu 30 katika Kijiji cha Ilembo,Wilayani Chunya Mkoani hapa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani hapa Barakiel Masaki,amesema kuwa tukio hilo limetokea Julai 17 mwaka huu majira ya saa kumi na mbili jioni wakati polisi wakiwa katika doria.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Richard Kalinga (17) na Ibrahimu Kabujo (19) wote ni wakazi wa Irembo wilaya ya Mbozi.

Ameongeza kuwa watuhumiwa hao wamekutwa na bangi hiyo wakiwa wamehifadhi katika mfuko aina ya sandalusi.

Aidha Kamanda Masaki amesema kuwa watuhumiwa hao ni watumiaji na wauzaji wa bangi ambapo suala hilo ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi.

Hata hivyo Jeshi la Polisi limetoa onyo kwa jamii kutojihusisha na matumizi ya kulevya kwani kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na pia kuatarisha maisha.

Post a Comment

 
Top