Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Katika hali isiyoyakawaida Mbwa mmoja asiyefahamika mmiliki wake,amevamia nyumba ya Bwana Michael Nkeka(52) ambaye Mkazi wa Nsalaga Uyole,Jijini Mbeya na kulala kitandani.

Tukio hilo limetokea Julai 12 mwaka huu majira ya saa 1 jioni,wakati mmiliki huyo akiwa amerejea nyumbani kutoka matembezini alifungua mlango wa nyumba yake ndipo Mbwa huyo alipoingia ndani na kupitiliza moja kwa moja mpaka chumbani kisha kulala.

Juhudi za kumuondoa mbwa huyo ziligonga mwamba ndipo Bwana Nkeka alipoamua kwenda kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Mtaa,Bwana Peter Ngonde ambapo hakukuwa na mafanikio yoyote hali iliyowapelekea kufikisha taarifa katika Kituo cha Polisi Uyole.

 Aidha,Polisi wa kituo hicho walieleza kuwa wamuache mbwa huyo huenda akaondoka mwenyewe lakini hali ikawa ndivyo sivyo kutokana na kulala mpaka asubuhi majira ya saa 3 ya Julai 13 mwaka huu.

Hata hivyo tukio hilo la aina yake limehusishwa na imani za kishirikina na hakuna tukio lolote la kuhatarisha.

Wakati huohuo mtoto mmoja Edrick Mwashiuya(2),mkazi wa Kijiji cha Halambo,Kata ya Halumbu Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya amefariki dunia baada ya kudondokea katika uji wa moto uliotengenezwa maalum kwa ajili ya kutengenezea pombe ya kienyeji.

Diwani wa kata hiyo Samson Simkoko amethibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea majira ya saa asubuhi ya Julai 13 mwaka huu na kwamba Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio kwa uchunguzi.

Post a Comment

 
Top