Menu
 


Chege amepata ajali maeneo ya Temeke Jana 16 July mida ya saa nne na nusu. Ajali imesababishwa na mwendesha pikipiki ambaye alikuwa amelewa sana na ameiba pikipiki alio kuwa anaendesha.Mwenye pikipiki alifika hospitalini na kusema alikuwa akijitayarisha kuwasha pikipiki yake huku akiva koti kwa ajili ya kujizuia na baridi ndipo alipo sukumwa pembeni na mlevi huyo na kuibiwa pikipiki yake . Kwa mwendo wa kasi sana pikipiki hio iliingia barabarani bila kujali magari wala usalama. 

Chege amepata maumivu makali kwenye mkono wake wa kushoto na ameshapata matibabu hospitali ya Kinondoni mida ya saa sita usiku.
 
Kabla ya ajali chege alikuwa studio akitayarisha CD Ya show atakayo kwenda kufanya Kigoma pamoja na kigoma  All star tarehe 17 July 2012. Baada ya kutayarisha hio CD Alikuwa aje kinondoni kujitayarisha na safari yake ya Kigoma mapema asubuhi.

Mskilize chege kwenye power jams ya tarehe 17, july 2012 Chege akitoa taarifa kwa marafiki kuhusu ajali na kwamba ametoka salama

 Chege akiwa na rafiki yake aliye msaidia baada ya ajali wakitoka kinondoni hospital baada ya kupata matibabu na dawa .

Kwa hisani ya Sammisago Blog!!.

Post a Comment

 
Top