Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mwimbaji wa nyimbo za Injli mkoani Mbeya Bwana Yona Mwaisango amekanusha kufumaniwa akiwa na mke wa mtu katika mtaa wa Ilolo Kati,Jijini Mbeya Julai 2 mwaka huu majira ya saa 2:30 usiku.

Mwimbaji huyo amesema hiyo ilikuwa ni mbinu tu zilizopangwa ili kumchafua yeye kwani alifika nyumbani hapo(inapodaiwa alifumaniwa) kwa lengo la kumsaidia hudumua ya chakula  na mpango wa kuwaelimisha ili waweze kukopa katika Shirika la mikopo la PRIDE .

Ameongeza kuwa alidaiwa pesa za ugoni shilingi laki tano na kuziahidi kulipa Julai 3 mwaka huu ambapo alitoa jumla ya shilingi 250,000 na kuahidi kiasi kilichobaki atakilipa Julai 7 mwaka huu.

Mwimbaji huyo amekiri kusaini barua ya kulipa faini hiyo na kwamba alifanya hivyo ili kuepuka kudhurika kutokana na kutishiwa usalama wake kutoka kwa wananchi wenye hasira kali na kwamba kwa sasa hayupo tayari kuzilipa pesa hizo kwani hakutenda kitendo hicho cha ugoni na cha aibu.

Aidha kikao hicho kilifanyika katika nyumbani hiyo(inayodaiwa alifumaniwa humo) kilichochukua muda wa masaa mawili kabla ya kuruhusiwa kutoka.

Hata hivyo,wimbi la watumishi wakubwa na kashfa ya ugoni na ubakaji zimezidi kuwaandama waimbaji mkoani hapa ,ambapo hivi karibuni Uncle Machibula alidaiwa kumbaka mwanafunzi wa Kidato cha Pili na kushikiliwa kwa siku kadhaa na kisha kuachiwa huru na Jeshi la polisi mkoani hapa.

Post a Comment

 
Top