Menu
 

Kituo kipya cha Sanaa kinachofahamika kwa jina la SWAGGA FIJHO kimeanzishwa katika jiji la Mbeya kwa lengo la kuwakutanisha vijana wenye vipaji na kuwaendeleza katika sanaa . Katika kituo hiki vijana wenye vipaji mbalimbali kama vile kudance, muziki, waigizaji, wachoraji, watayarishaji muziki wanapatiwa mafunzo ya sanaa bure na mafunzo mengine yatakayotolewa katika kituo hiki ni Kompyuta kama vile teknolojia ya mawasiliano (Internet, Graphic Design),utayarishaji wa filamu na pia watapatiwa fursa mbalimbali katika ulimwengu wa sanaa. 

Lengo lingine la kituo hiki cha Sanaa ni kuwaunganisha wasanii wa Mbeya na wasanii mbalimbali wa Tanzania pamoja na wasanii kutoka nje ya nchi.

SWAGGA FIJHO Arts Centre ni kitovu cha Sanaa na Ubunifu na kipo kwa ajili ya shughuli mbalimbali kama vile mafunzo, kuandaa maonyesho, warsha, uzalishaji wa kazi za Sanaa na ubunifu, utoaji maelezo mbalimbali kuhusu sanaa na wasanii na pia kufanya tafiti mbalimbali za sanaa na utamaduni.


Kituo hiki kimeanzishwa kwa lengo la kuwasaidia vijana wenye vipaji ambao hawapatiwi fursa ya mafunzo na kuendelezwa katika sanaa na ubunifu ambapo mkoa wa Mbeya unasifika kwa kuwa na vijana wengi wenye vipaji mbalimbali.

Post a Comment

 
Top