Menu
 

Na Ester Macha, Mbeya.
Katika maisha ya mwananchi kila mmoja anapaswa kujishughulisha na kilimo cha mazao mbalimbali ili aweze kuendesha maisha yake hususani kusomesha watoto.

Katika kufanikisha hili serikali imekuwa ikitilia mkazo suala la kilimo kwa wananchi waliopo vijijini na Mjini ili kuweza kukabiliana na njaa  katika jamii ambayo imekuwa ikitokea  kwa wananchi hasa waishio vijijini ambao kwa kiasi kikubwa wao ndo wamekuwa wakikubwa na adha hiyo.

Wananchi wamekuwa na jitihada zaa kuhakikisha wanalima na kupata mazao bora ambayo yanaweza kuwazesha kupata masoko ya uhakika kutokana na ubora unaokuwepo katika mazao yao, lakini pia hata suala la pembejeo ambalo ni muhimu kwa mkulima ili aweze kuvuna mazao mengi kutokana na kutumia njia za kisasa.

Hivi karibuni mwandishi wa makala haya alitembelea Mashamba ya Vitunguu  maji yaliyopo katika Kata ya Igomelo wilaya ya Mbarali kuona shughuli zinazofanywa na wakulima hao na  kujishughulisha na kilimo cha vitunguu ambacho nkimekuwa kikilimwa kwa wingi katika Wilaya hiyo.

Kilimo hicho cha vitunguu ambacho kimekuwa kikilimwa kwa njia ya umwagiliaji kimekuwa kikileta  tija kwa wakulima licha ya kuwa vitunguu vimekuwa havina soko na hivyo kubaki kuuza kwa bei ya chini,na hata kwa upande wa  pembejeo imekuwa tatizo kutokana kuuzwa kwa bei  juu na hivyo kuwalazimu wakulima kushindwa kununua pembejeo hizo.

Akizungumza na gazeti hili mmoja wa wakulima wa Skimu ya umwagiliaji
ya Igomelo Bw.Daudi Kidange anasema kuwa  katika kilimo hicho wamekuwa wakilima kwa nguvu nyingi lakini tatizo limekuwa ni soko kwao na hivyo kulazimika kuuza kwa bei ya chini licha ya kutumia nguvu nyingi.

Anasema kuwa licha ya kilimo hicho cha umwagiliaji kuwa kizuri lakini bado kuna tatizo la soko la vitunguu kwa wakulima hao.

“Kupitia hiki kilimo cha umwagiliaji mimi nalima Mihogo,Mahindi pamoja na nyanya lakini zao langu kuu ni vitunguu tu ambavyo vimekuwa vikinisaidia kuendesha maisha yangu na familia yangu haya mengine ni ya ziada tu”anasema Mkulima huyo.

Mkulima Mwingine Bw.Gerald Mwalongo anasema kuwa kupitia kilimo cha vitunguu amepata manufaa makubwa kwasababu kwa mwaka analima mara tatu kwa mazao tofauti lakini kitunguu ndo zao pekee ambalo linafanya aendeshe maisha yake.

Anasema kuwa hapo nyuma hawakuwa  na uwezo wa kusomesha  watoto lakini baada ya kuanzqa kilimo cha vitunguu wameona manufaa kutokana na watoto wao kusoma na hata kuendesha maisha yao ambayo awali hayakuwa mazuri na kusema kuwa toka ameanza kilimo hicho ana miaka minne  na mpaka sasa anaendelea na kilimo cha vitunguu.

“Sawa tunalima na mazao mengine lakini tegemeo kubwa hapa ni kilimo cha  vitunguu ambapo  wote tuliopo kwenye hii skimu ya umwagiliaji asilimia kubwa ni kilimo cha vitunguu  ambacho ni tegemeo kubwa kwa sisi wakulima”anasema.

Akizungumzia kuhusu changamoto za kilimo hicho Bw.Mwalongo anasema kuwa pembejeo imekuwa ni tatizo kubwa kwa wakulima  kutokana na bei kupanda kila siku  hivyo kumfanya mkulima wa hali ya chini kushindwa kumudu pembejeo hizo.

Mkulima huyo anasema kuwa   kutokana na pembejeo hizo kuwa bei juu ni vema serikali ikachunguza ushuru ili kuweza kuingiza bila ushuru ili wakulima waweze kununua kwa bei ya chini.

Akiongelea kuhusu Soko la Vitunguu  Bw. Mwalongo anasema hawana soko maalamu la kuuzia vitunguu kwani wakishalima wateja wanakuja shambani moja kwa moja kwa kununua bei yeyote wanayotaka wanunuzi hao,kwa sehemu kubwa wao ndo wapangaji wa bei kwasababu bei ikipangwa na wakulima wenyewe wanakuwa hawaridhiki.

Kufutia kukosa Soko hilo anasema mara nyingi wamekuwa wakiomba serikali iwatafutie soko la vitunguu lakini bado hakuna kinachoendelea.

Hata hivyo anasema kuwa wanunuzi wa vitunguu hivyo wanatoka
Tunduma,Malawi,CongoRuvuma, kwa upande wa Dar ni mara chache kutokea.

Akizungumzia kuhusu bei  mkulima huyo anasema kwa gunia moja huuzwa kati ya sh.3,0000 mpaka 25,000 hali ambayo inaathiri maisha ya wakulima.

“Tunaomba serikali itusaidie kupata soko kwani kwa bei hii tunayouza
ni unyonyaji mkubwa ukijitahidi sana unauza sh.70,000 kwa gunia moja.

Mkulima mwinginwe Bi. Ashiza Mwogofi ambaye ni mkazi wa Igawa anasema kwa upande wa soko mwaka hadi mwaka hadi  vimekuwa havina soko.

Bw.Raphael Bendo anasema  tatizo  kubwa lililopo kwa wakulima ni gharama ya pembejeo na ukosefu wa soko hali hiyo inaathiri wakulima kutokana na wanunuzi kuja kwenye mashamba kwa pamoja hivyo inakuwa ngumu kwa mkulima kuwa na sauti ya pamoja.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Skimu  ya Umwagiliaji ya Igomelo Bw.Luhana Mpinga anasema skimu hiyo ina wanachama 315,wanachama wamekuwa wakijikomboa kupitia kilimo cha umwagiliaji lakini tatizo ni soko la vitunguu.

Tatizo kubwa lililopo ni kutokuwa  na soko la uhakika, maghara ya kutunzia mazao kwani yaliyopo si ya kisasa kuna umuhimu serikali ikawajali wakulima kwa sehemu fulani.

Hata hivyo anasema wafanyabishara wamekuwa wakiwarubuni wakulima kwa kuongeza ujazo kwenye magunia wakati serikali ilishakata mtindo wa LUMBESA.

Naye Ofisa Kilimo na Mifugo Wilaya ya Mbarali Bw. Dickson Maruchu
anasema wameanza kujenga miundo mbinu ya masoko ya vitunguu, katika maeneo ya Chimala,Mbuyuni,hata hivyo anasema wamewahamasisha wakulima wajiunge kwenye vikundi.

Aidha Bw. Maruchu anasema mwaka 2013 wanatarajia kujenga  visoko vidogo ambako kutakuwa na mashine za usindikaji  ili viweze kuwasaidia wakulima katika mazao yao wanayolima.

Post a Comment

 
Top