Menu
 

Mwenyekiti wa Bodi Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Dk.Norman Sigalla akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu kufukuzwa kazi kwa madaktari hao. 
 *********
Habari na Gabriel Mbwille,Mbeya.
Vijana nchini wametakiwa kujitambua na kujithamini ili waweza kujitegemea na namna ya kuyakabili maisha yao na siyo kujifanyia mambo ambayo hata hayaendani na vipaji vyao.


Rai hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya  Dokta Norman Sigalla wakati akifungua Kongamano la Jukwaa la vijana lililoandaliwa na Asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Msingi wa Maisha ya Amani na kufanyika katika ukumbi wa Mkapa.


Aidha amesema ili kijana aweze kukabiliana utandawazi wa maisha ya sasa ni lazima ajitambue mwenyewe thamani yake na kutathimini nini anaweza kufanya katika maisha yake na siyo kukimbilia fani ambayo haiendani na kipaji chake.


Ameongeza kuwa maendeleo yoyote katika taifa lolote yanategemea uwepo wa mtu mwenye hekima na busara katika kuamua kufanya jambo hususani kwa kijana wa leo.

Post a Comment

 
Top