Menu
 

Habari na Angelica Sullusi,Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro,amewataka wakazi wa Mkoa huo kufuata utaratibu wa kitabibu wa rufani ili kupungunza msongamano mkubwa unaoweza kujitokeza katika hospitali za Rufaa na Mkoa kwa kutibiwa katika Vituo vya Afya badala ya kukimbilia hospitali kubwa.

Wito huo ameutoa jana katika Hospitali ya Rufaa Mbeya wakati wa ziara yake kuzungukia Hospitali za Mkoa huo ili kuangalia hali ya utoaji huduma kwa wagonjwa baada ya kuwepo kwa mgomo wa madaktari.

Akizungumzia uhakika wa huduma kwa niaba ya Serikali  Kandoro anasema: “Napenda kuwahakikishia wananchi kuwa licha ya kuwepo kwa upungufu wa madaktari serikali inaendelea kufanya utaratibu kuhakikisha huduma hii inarejea kama ilivyokuwa hapo awali,”.

Aidha,ametumia nafasi hiyo kuwasihi wakazi wa Mbeya hususani akina mama wajawazito ambao wanahitaji huduma ya kujifungua kwa njia ya kawaida kuvitumia vituo vya afya vya Luanda,Igawilo,Iyunga na Kiwanjampaka vilivyopo katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya ili kutoa mwanya kwa wenzao wenye kuhitaji uangalizi maalum kuhudumiwa ipasavyo katika hospitali kubwa.

“Lakini nitoe wito kwa wakazi wa mbeya kuvitumia vituo vyetu vya afya kwa wagonjwa ambao hawana matatizo makubwa ili kupunguza msongamano katika hospitali hii na hivyo kuwapa nafasi ya kutibiwa kwa haraka wenzetu wenye matatizo hasa wale wa dharura kama ajali,”.

 Mkuu huyo wa Mkoa pia ametembelea Hospitali ya Wilaya ya Mbeya Ifisi,Hospitali teule ya Igawilo pamoja na hospitali ya Mkoa ambapo alijionea hali ya mlundikano wa wagonjwa hususan wagonjwa wa nje(OPD),na kuelezwa changamoto kadhaa zilizojitokeza hospitalini hapo kutokana na mgomo wa madaktari.

Post a Comment

 
Top