Menu
 

Habari na Mwandishi wetu.
Watoto wanne wa familia moja wamemuua baba yao Bwana William Mwakwama(68),mzazi kisha kumchoma moto wakimtuhumu kujihusisha na imani za kishirikina katika Kitongoji cha cha Ibolefa,Kijiji cha Itota,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Diwani Athuman,amesema tukio hilo limetokea majira ya saa mbili asubuhi Juni 28 mwaka huu na kwamba chanzo cha mauaji hayo ya kikatili ni tuhuma za kishirikina baada ya kumtuhumu kumuua kwa kumloga mjukuu wake.

Amewataja watoto hao waliohusika na mauaji ya baba yao ni pamoja na Samwel Mwakwama(38),Dickson Mwakwama(25),Ambakisye Mwakwama(20) ambao wote ni wakazi wa Airpot jijini Mbeya na Rodrick Mwakwama(28) mkazi wa Kasumulu,Wilaya ya Kyela.


Kamanda Diwani,amebainisha kuwa watuhumiwa wamekamatwa na upelelezi wa tukio hili unaendelea,pia ametoa wito kwa wananchi kujiepusha na imani za kishirikina na kuacha tabia za kujichukulia sheria mikononi ambazo huleta uvunjifu wa amani ndani ya jamii.

Kwa siku za hivi karibuni kuwekuwa na matukio ya wananchi kujichukulia sheria mkononi hasa yakihusishwa na imani za kishirikina ambapo Jeshi la Polisi,MJATA na Viongozi wa kidini wamekuwa wakikemea hasa kwa kutumia dhana ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.

Post a Comment

 
Top