Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga.
Wanawake watatu wa familia moja wamezirai baada ya kunyweshwa dawa na Mganga wa Kienyeji walikokwenda kuagua katika Kitongoji cha Mikocheni,Kijiji cha Namambo,Kata ya Totowe,Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya.

Tukio hilo limetokea Julai Mosi mwaka huu,ambapo wanawake hao walikwenda kwa Mganga wa kienyeji Bwana Lushinga kwa lengo la kuagua wakitaka kufahamu kwanini mama yao mwenye umri wa miaka 75 haoni na anasumbuliwa na ugonjwa wa macho kwa muda mrefu.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Namambo Bwana Zacharia Mwandanji,amethibitisha tukio hilo na kuwataja wanawake hao kuwa ni pamoja na Bi.Emaculate Gibson,Tatu Gibson na Nampomwa.

Baada ya kunywesha dawa na mganga huyo wanawake hao walizirai mara moja na kuzinduka baada ya siku tatu Julai 3 mwaka huu,majira ya saa saba mchana huku wakiwa hoi kwa uchovu.

Aidha,imani za kishirikiana zimekuwa chanzo cha mauaji mengi mkoani hapa,tabia ambayo imelaaniwa vikali na asasi mbalimbali zikiwemo za Muungano wa Jamii Tanzania(MJATA) na Jeshi la Polisi kupitia ulinzi shirikishi.

Hata hivyo wananchi wametakiwa kujiepusha na waganga wanaosababisha uvunjifu wa amani katika jamii.

Post a Comment

 
Top