Menu
 

Mkali wa Hits Song kama Domolangu,Waleo Wakesho na Samson na Delila inayofanya vema kupitia Radio station mbalimbali nchini TIMBULO ,kuibiwa kamera yake kumbwa aina ya Sony aliyoinunua kwa Dola 800 za Kimarekani,kusogezewa ama lugha nyingine kuibiwa wakati wa Party  ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.nazungumzia siku ya Jumamosi ya Julai 7  2012 iliyofanyika nyumbani kwao katika Kijiji cha Ruiwa Ijumbi,Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.
Chimbuko Letu Blogu!! Ilipata kushuhudia Msanii Timbulo  akiwa hana la kufanya baada ya kubaini kuwa kachezewa mchezo mchafu baada ya kamera hiyo iliyokuwa ikishikwa na kila ambaye anauwezo wa kuitumia kuendelea kupokezana kutokana wengi wao kung'ang'ania kupiga picha na nyota huyo huku karibia nyomi nzima likiwa limechangamka kupitia swaga za mitungi walizokuwa wamejitupia na kuparty kwa furaha na mwana..
Pichani Msanii Timbulo akiwa na Bi.Mkubwa wake pande za Ruiwa Ijumbi kabla ya show.

Aidha msanii huyo amesema juhudi zinaendelea ili kuweza kumbaini mhusika aliyemsogezea kamera hiyo,na msako upo makini kutokana na kuwa sehemu kubwa ya umati uliohudhuria party hiyo unafahamika kutokana na kuwepo kwa mtandao wa kupokezana,licha ya kuwepo kwa tabia ua kila aliyekuwa akishika kumtupia mzigo mwenzie kwamba mimi nilipomaliza kupiga picha nilimpa mtu fulani.
 
Hata hivyo party hiyo iliyohudhuriwa na maelfu ya watu na kukata keki ya Happy Birthday Timbulo,Chimbuko Letu Blogu ilishuhudia Jukwaa likishindwa kuhimili mikito ya uchezaji wa Timbulo na Wacheza show wake kufuatia watu wa kijijini hapo kushindwa kuvumilia kutokana na kupandwa na mzuka wa msanii huyo kutokana na ukame wa burudani unaowakabili kwa muda mrefu,kisha watu hao kuonekana kupanda jukwaani na mwisho wa siku kuzungumza kwa kusalimu amri ya kuvunjika.

Wakati huo huo moja ta tukio lililojitokeza ni pale Diwani Mdimilaje,alipolazimika kuingilia kati utata uliokuwepo kufuatia kuwepo kwa mvutano baina ya Afisa Mtendaji wa Kata na Timbulo kuzuia Party hiyo kufanyika na kucheleweshwa baada ya mchana na kuwa usiku.
Sehemu ya Nyomi la wakazi wa Kijiji cha Ruiwa Ijumbi,Wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya waliojitokeza kwa wingi katika Party ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake msanii Timbulo.
 Siku moja kabla ya Show Timbulo alitimba katika Studio za 104.0MHz Bomba FM Radio iliyopo mkoani Mbeya.

Post a Comment

 
Top