Menu
 

Na Bosco Nyambege,Mbeya
Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linamtafuta mtu aliyehusika na kitendo cha kumwiba mtoto mwenye umri wa miezi miwili katika Kijiji cha Manga Madibira Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa polisi Mkoani hapa Diwani Athumani amesema kuwa tukio hilo limetokea mnamo Julai 18 mwaka huu majira ya saa kumi jioni.

Amemtaja mama wa mtoto huyo kuwa ni Bi.Tabu Chapunga(18),mkazi wa mkunywa na aliibiwa mtoto wake aitwaye Gulo Manga wakati mama yake akiwa amekwenda kuchota maji.

Aidha,amesema kuwa mtu huyo aliingia chumbani kwa mama huyo na kumchukua kichanga hicho na kutokomea nacho kusiko julikana.

Hata hivyo Kamanda Diwani ametoa mwito kwa mtu yeyote mwenye taarifa juu ya mhusika wa tukio hilo ili kuweza kumbaini mtuhumiwa huyo na kufikishwa katika vyombo vya dola.

Post a Comment

Michael Minja said... 21 July 2012 at 02:47

Dah hii nayo ni habari ya kusikitisha sana na sijui alikuwa na lengo gani la kuamua kufanya kitu cha namna hii au ndio imani za kishirikina.

 
Top