Menu
 

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abas Kandoro wa kwanza kulia,akifuatiwa na Mgeni Rasmi Dr  Christina Shengoma,ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakifuatilia kwa umaniki matukio mbalimbali katika Kilele cha Maadhimisho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ndani ya Viwanja vya John B. Mwakangale jana. Kauli mbiu ya siku ya Wakulima na wafugaji “Nane Nane” kwa mwaka huu ni "KILIMO KWANZA ZALISHA KISAYANSI NA KITEKNOLOJIA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU"
 Haya ni Mambo yale ya nyama choma ndani ya Viwanja vya John B. Mwakangale nane nane.
 Mdau akiwa anaweka sawa kitu cha nyama choma.


 Ndani ya banda la Chuo cha Mbeya Institute of Science and Technology(Mist),katika Viwanja vya John B. Mwakangale.

 Ni Jengo la Mamlaka ya maji hapa 
Mgeni  Rasmi Dr Ishengoma,Mkuu wa Mkoa wa Iringa.

Baadhi ya wananchi kutoka taasisi mbalimbali wakiwa katika maandamano katika maonesho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika Viwanja vya John B. Mwakangale mkoani Mbeya.
Baadhi ya wananchi kutoka taasisi mbalimbali katika maonesho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika Viwanja vya John B. Mwakangale mkoani Mbeya.
 Wananchi na wadau kutoka taasisi mbalimbali wakitazama maandamano katika maonesho ya sikukuu ya wakulima na wafugaji nanenane Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwa katika Viwanja vya John B. Mwakangale mkoani Mbeya.ndamano hayo ya maonesho
 Kauli mbiu ya siku ya Wakulima na wafugaji “Nane Nane” kwa mwaka huu ni "KILIMO KWANZA ZALISHA KISAYANSI NA KITEKNOLOJIA ILI KUKIDHI MAHITAJI YA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU"
 Pembejeo kibao zinapita hapa.
 Mgeni Rasmi Dr Christina Shengoma akihutubia wakulima pamoja na wananchi wote wa mikoa inayounda Kanda ya Nyanda za Juu Kusini ikiwa ni pamoja na Iringa,Mbeya,Rukwa,Katavi na Njomba katika sikukuu ya wakulima na wafugaji nanenane.
 Burudani ya Ngoma za asili enzi na jifunze utamaduni wa kabila lako,ili kuendelea kuudumisha utamaduni wa mtanzania.

 Akina mama wakiwa wamevalia mavazi ya Chama tawala yaani Chama Cha Mapinduzi(CCM) nao hawakuwa nyuma ili mradi ni mkereketwa na unapendezewa na sera zake..
 Lile Gari linalotumia Mtungi wa Gesi kutoka MIST ndilo linapita sasa 

 Mwandishi wa habari na mpiga picha wa Kituo cha Televisheni cha ITV Ndugu Festo  akiwa anachukua kwa makini Ngoma za asili katika maonesho ya nane nane.
Picha zote zimepigwa na Ndugu Joseph Mwaisango(Mbeya Yetu Blog.)

Post a Comment

 
Top