Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbeya.
Mtu mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja anayedaiwa kuwa ni mkazi wa Nambala,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya ameuawa na kisha kuchomwa moto na kuteketea mwili mzima kwa kile kinachodaiwa kuwa marehemu huyo amekuwa akijihusisha na vitendo vya ubakaji.

Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili asubuhi katika Kijiji cha Masangula,Kata ya Nyimbili,wilayani humo siku ya jana Agosti 9 mwaka huu,ambapo marehem.

Marehemu anakadiliwa kuwa na umri kati ya miaka 25 mpaka 30,ambapo wakazi wa kijiji hicho wamedai kuwa marehemu amekuwa akijihusisha na vitendo hivyo vya ubakaji kijijini hapo kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Asalile Mbembela,ambaye amesema tukio hilo ni la mara ya kwanza kutokea kijijini hapo.

Aidha,Afisa Mtendaji wa kijiji hicho Bwana Elinga Kalinga,alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi Mbozi,hata hivyo hakuna mtu hata mmoja aliyejitokeza kuhusiana na tukio la ubakwaji.

Kwa upande wake Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa Diwani Athuman,amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo na kutoa wito kwa wananchi kutojichukulia sheria mkononi,hali inayopelekea kusababisha mauaji.

Hata hivyo amesema pindi wanapomkamata mhalifu au mtuhumiwa wamfikishe kwenye vyombo vya sheria ili kuchukua mkondo wake  na kwamba wananchi wanapaswa kuwa waadilifu kwa kufuata imani zao ambapo zitasaidia kupunguza uhalifu mkoani hapa.

Post a Comment

 
Top