Menu
 

FFU wa Ngoma Africa band kuvamia maonyesho makubwa International African  Festival ,Tubingen 11.08.2012

Pia watapokea tuzo ya Bendi bora ya kiafrika barani ulaya

Ngoma Africa band aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani,Bendi hiyo maarufu barani ulaya itatingisha tena jukwaa la onyeshoya kimataifa la International African festival ,mjini Tubingen,Ujerumani.siku ya jumamosi 11-08 na jumapili 12-08-2012 katika uwanja waFestPlatz, TubingenHabari za uhakika zinaeleza kuwa bendi hiyo imechaguliwa kuwabendi bora ya kiafrika barani ulaya na kushinda tuzo la Award ya
"IDA - International Diaspora Award". 
Tuzo hiyo itakabidhiwakwa kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki mahiri Kamanda Ras Makunjausiku wa Jumapili 2012,Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kimepigiwa
kura nyingi na washabiki,pamoja na tahasisi mbali mbali kwa kutajwa kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyoweza kutumia muziki wake kama daraja na kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki na kuwaunganishawashabiki wa mataifa mbali mbali duniani.
Pia kikosi kazi hiko kimetajwa  mara nyingi kuwa kimediliki kujitoa muanga kwa
kupiga muziki mpaka kwenye nchi zenye usalama mdogo na mazingira ya kivita !
kwa ujasili huu Ngoma Africa band inavuna inachopanda

Ngoma Africa band imetajwa kuwa muziki wake umefanikiwa kuzoa mamilioni
ya washabiki na kuchangia kwa kiasi kikubwa kutukomeza fikira za kiubaguzi wa
rangi zilizomo kwa baadhi ya wazungu barani ulaya.

Ngoma Africa band inasemekana kuwa na washabiki au wafuasi milioni 50
dunia nzima,na washabiki wengine milioni 11 wanapitia tovuti ya bendi
hiyo at http://www.ngoma-africa.com au www.ngoma-africa.com

miongoni mwa wapenzi hao ni wapo wanawake na wanaume ,
watoto ,vijana na wazee wenye rika na mataifa mbali mbali,
bila kujali itikadi za dini na matabaka ya maisha yao,wote wapo
chini ya kivuli cha mzuka wa muziki wa Ngoma Africa Band aka FFU
inayoongozwa na kamanda Ras Makunja aliyepindia akili kazi yake !

Tusikose kuwasikiliza FFU at www.ngoma-africa.com

Post a Comment

 
Top