Menu
 

IMEANDIKWA NA MWANDISHI ADELA
Kitanda usichokilalia ,huwezi kujua kunguni wake ,shida na mateso wanayoyapata watoto waishio katika mazingira hatarishi na wale wa mitaani ni vigumu kueleza. Watoto hawa hawajui leo au kesho watakula nini ,hakuna anayeangaika kuwatafutia chakula ,wanapolala na njaa hakuna wa kumlilia na wakiumwa hakuna wa kumweleza hivyo huendelea na maisha yao hadi wanapopata nafuu au kupona kabisa.
     Ukweli na kwamba ,watoto hawa hujisikia wapweke kutokana na jamii kubwa kuwakataa na kuwaweka katika fungu tofauti. Jambo la kusikitisha ,idadi kubwa ya watoto umri wao unaanza miaka miwili hadi kumi ambao kimsingi hawajui kujitegemea ,njaa ikiuma wanalia tu na kushindwa kujieleza. Kitanda chao ni barabarani na wengine mitaroni ,baridi yote ya usiku na jua la mchana ni lao ,hawajui kubadilisha nguo,zile walizovaa wiki iliyopita hadi leo hazijatoka mwilini,  Tumezowea kuwaona watoto wenye wazazi wakitoka nyumbani asubuhi na kurudi majumbani mwao jioni .Watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi hawana pa kwenda ,popote wanalala.  Jamii imesahau kuwa watoto hawa ni sawa na wao ,wanasikia njaa ,baridi na maumivu sawa na wenzao lakini nani anashughulika nao?
    Watoto hawa hawakuchagua kuwa yatima na kuishi mitaani ,hawakuchagua kufiwa na wazazi wao ,wamejikuta wapo mitaani na hawana la kufanya kama watoto wetu wanavyojikuta wakiwa mikononi mwetu na wanapata kila kitu. Waswahili wanasema ,kinga ni bora kiliko tiba .Mashirika yasiyo ya kiserikali NGOs na yale ya kimataifa kama UNICEF na Serikali ,wanashughulikia tatizo la watoto hawa wakiwa tayari mitaani . Jambo la msingi ,nguvu inayotumika kuwasaidia watoto hawa ingepaswa kuelekezwa kwenye kinga ili kutibu tatizo hilo kabisa.Sababu moja wapo inayochangia ongezeko la yatima na watoto wa mitaani ni migogoro isiyokwisha  katika ndoa.
      Hatua za haraka zinahitajika ili kupunguza au kumaliza tatizo la watoto wa mitaani  na yatima kwa kuwaunganisha na walezi pamoja na ndugu zao ambao tunaamini wapi.
      Umefika wakati wa serikali kuratibu nguvu za NGOs kwa kuhakikisha mashirika hayo,jamii na wao wenyewe wanachukua hatua stahiki  kuhakikisha tatizo hilo nchini linakwisha...

Post a Comment

 
Top