Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Mbozi.
Katekista wa Kanisa Katoliki Kijiji cha Ikonya,Kata ya Bala,Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya Bwana Amon Msokwa(40),Agosti 19 mwaka huu amefunga pingu za maisha(ndoa) na mke wa mtu Bi Melina Mbonda(34) ambaye pia ni mama wa watoto wanne.

Inadaiwa awali Bi Melina aliolewa na Shadraka Mwendawila Mkazi wa kijiji hicho hicho na kujaaliwa kupata watoto wanne.

Harusi hiyo ilifungwa siku ya Jumapili majira ya 5 asubuhi na Padre Mpiga Uzi,lakini majira ya saa 6 mchana kulitokea taflani ambapo Bwana Shadraka alijitokeza na kupinga ndoa hiyo isifungwe kwa madai kuwa ni mke wake na wana watoto wanne.

Kufuatia sakata hilo ndoa hiyo haikustahili kufungwa.

Hata hivyo Bwana Shadrack aliondolewa eneo la Kanisa na ndoa ikafungwa manamo majira ya saa 8 mchana na Padri Mpiga Uzi.

Post a Comment

 
Top