Menu
 

Hakimu wa mahakama ya mwanzo Mwanjelwa JP MWAMBAPA ameitaka jamii kutumia mabaraza ya kata na mitaa katika kusuhisha kesi za kifamilia na madai ili kutoa nafasi kwa mahakama kusikiliza kesi ambazo zimekuwa vigumu kuamriwa na mabaraza hayo.

Aliyasema hayo wakati wa mahojiano na mtandao huu ofisini kwake na kudai kuwa kesi nyingi zimekuwa zikishindwa kufikiwa muafaka kutokana na wanafamilia wenyewe kushindwa kuyatumia mabaraza ya kata.

Aidha MWAMBAPA alizitaja baadhi ya kesi zinazoongoza kusikilizwa mahakamani hapo kuwa ni kesi za mirathi, talaka na madai ambapo kwa sehemu kubwa zimekuwa ni vigumu kutolewa hukumu kutokana na walalamikaji kutopitia kwenye mabaraza ya kata pamoja na vyombo vya dini.

Hata hivyo alisema chanzo cha kesi hizo ni mmomonyoko wa madili ndani ya jamii.

Post a Comment

 
Top