Menu
 

Marehemu Rehema Kiyenga,enzi za uhai wake.

Msaada kwa Mkazi yeyote wa Mkoa wa Iringa anaiyeifahamu familia ya Marehemu Rehema Kiyenga,tunaomba taarifa hizi ziwafike. Cheti cha kuzaliwa jina la baba yake ana jina la Lupembe wa Mkoa wa Iringa.

Rehema Kiyenga ameishi nchini Marekani kwa muda wa miaka mingi na amefariki dunia kama mwaka hivi na mwili wake ulizikwa kwa utaratibu walionao Marekani baada ya ndugu zake kushindwa kujulikana.

Mwisho!!
Kama unaweza kuuliza hapo Iringa kwa yeyote anayemjua au kuifahamu familia yake au ndugu zake ili kuweza kupata taarifa kutokana na ndugu kutafutwa bila mafanikio.

Mungu ailaze roho ya Marehemu Rehema Kiyenga, mahali pema peponi Amina.

Imetumwa na Baba Jaheim Abdul Jaha Mlanzi
Mdau wetu kutoka Marekani.

Post a Comment

Michael Minja said... 10 August 2012 at 01:43

Dah hii inasikitisha sana hasa kwa sisi tunaokaa nchi za watu inatubidi tuwe tunatoa taarifa hasa kwa watu wakaribu yetu ili tunapoweza kupata matatizo basi tuweze kusaidiwa hasa kwa tatizo kama hili lililompata Dada yetu. Ee Mungu ipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi amina.

 
Top