Menu
 

Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe Mbeya.
Mtoto anayefahamika kwa jina la Allan Mwakalasya(17),mkazi wa Kijiji cha Mpandapanda,Kata ya Kiwira,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya amehofiwa kufa maji baada ya kwenda kuogelea katika maporomoko ya Mto Kiwira.

Tukio hilo limetokea Julai 6 mwaka huu majira ya saa 6 mchana, marehemu akiwa na mwenzake walienda kuogelea katika maporomoko ya mto huo,ndipo alipopiga mbizi mara tatu na mara nne aliingia akiwa ametanguliza kichwa alichukua dakika tano kuibuka na kunyosha mikono juu na kuzama moja kwa moja na mpaka sasa hajapatikana.

Baada ya tukio hilo watoto wenzake walichukua jukumu la kwenda kutoa taarifa kwa mama yake mzazi Bi. Emma Kosiyo(43) na mjomba wake Bwana Albert Mwakajila(60),ambao walienda eneo la tukio na kumtafuta Allan bila mafanikio na kuamua kutoa taarifa katika Ofisi ya kijiji ambapo ilipigwa Mbiu na wananchi kukusanyika eneo hilo la tukio huku wataalamu wa uzamiaji majini wakimtafuta bila mafanikio.

Takribani siku wananchi wameendelea na zoezi hilo na wakati huo wanatarajia kuonana na Viongozi wa kimila ili kusaidia kuendelea kuutafuta mwili wa Allan.

Hata hivyo taarifa hizo zimetolewa katika Kituo cha Polisi cha Kiwira,na Askari wa kituo hicho wameendelea kushirikiana na wananchi kuutafuta mwili huo.

Post a Comment

 
Top