Menu
 

Mtu mmoja anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi Kichwani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia Risaasi za moto na mabomu ya machozi waandamanaji wa Chadema mjini hapa.

Baadhi ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa jana. Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya machozi.
 Huyu ni Ally Zona muuza magazeti wa Msamvu Morogoro akiwa hajitambui baada ya kutandikwa risasi na Polisi kuzuia maandamano ya CHADEMA

Source: The Choicetz.blogspot.
Daima panapotokea vurugu au vita wanao athirika zaidi ni akina mama na watoto, na hii ndio hali hali ilivyokuwa hii leo mjini Morogoro ambapo Mama na mtoto, uchungu wa mwana aujuae mzazi, hapo kila mtu aliweza namna ya kujisalimisha na moshi wa mabomu ya machozi yalipokua yakiendelea kurindima.
                               Mmoja wa kiongozi wa Chadema akitiwa nguvuni wakati wa maandamano hayo yanaendelea wakati wakielekea katika uwanja wa shule ya Kiwanja cha Ndege.

Mkuu wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) BENSON KIGAIYA akiwa chini ya ulinzi wa gari la polisi mara baada ya kukamatwa wakati wa zoezi la kuwapokea viongozi wa juu wa chama hicho kushindikana katika eneo la Msamvu kwa ajili ya maandamano kuelekea kwenye mkutano wa hadhara wa Chadema shule ya msingi Uwanja wa Ndege mkoani Morogoro.

Kwa hisani ya mrokim.blogspot.com

Post a Comment

 
Top