Menu
 

Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa kila Mdau wetu/Msikilizaji wetu wa Kituo cha Redio cha kurushia matangazo BOMBA FM 104.0MHz MBEYA - TANZANIA kwa ushirikiano wenu,hii ni zawadi kwa wadau wote popote pale mlipo.

BOMBA FM REDIO imeibuka mshindi wa nafasi ya pili,huku TBC wakiibuka kama mshindi wa nafasi ya kwanza na MBEYA PRESS CLUB wakiwa katika nafasi ya tatu kwa Vyombo vya Habari vya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini katika kipengele cha MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA katika Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima na Wafugaji yaani Nanenane yaliyofanyika kikanda katika Viwanja vya John B.Mwakangale vilivyopo Jijini Mbeya.

Shukrani nyingine pia ziende kwa Viongozi wa mbalimbali wa Serikali Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wakiwemo Wakuu wa Mikoa,Wabunge,Wakuu wa Wilaya,Uongozi wa TASO,Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA),Taasisi mbalimbali,Vyombo Vya Habari na wafanyakazi wa vyombo hivyo pamoja na viongozi wengine wa Sekta mbalimbali,bila kuwasahau Wafanyabiashara na Wadau wote waliohudhuria maadhimisho hayo..

 *******
Imetolewa na Utawala kupitia Kitengo Cha Promotion.
Bomba FM 104.0MHz
Elimisha & Burudisha!!
+255 755 790 000
+255 656 117 664
Barua pepe:- bombafm104@yahoo.com

Post a Comment

 
Top