Menu
 

WILAYA YA CHUNYA - KUPATIKANA NA NYARA ZA SERIKALI.
MNAMO TAREHE 12.08.2012 MAJIRA YA SAA 19:30HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISANGAWANA WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. 

ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA ZUBERI S/O RAMADHANI,MIAKA 27,MMBONDEI,DEREVA WA GARI T.136 AHE MKAZI WA DSM NA STEVEN S/O EBRON,MIAKA 32,KYUSA MKAZI WA DSM WAKIWA NA JINO MOJA LA TEMBO LENYE UZITO WA KILO KUMI [10] .

MBINU NI KUHIFADHI JINO HILO KATIKA MFUKO WA SULPHATE NA KUFICHA KWENYE CABIN YA GARI HILO . WATU WENGINE WAWILI WALIOKUWA ABIRIA KATIKA GARI HILO AMBAO NI  ALFA S/O OMEGA,MIAKA 34,MKULIMA ,MUWANJI MKAZI WA KIJIJI CHA GUA NA SAVINUS S/O DARASI ,MIAKA 28,MKULIMA MKAZI WA GUA WAMEKAMATWA KWA MAHOJIANO. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA HUSIKA MARA WAONAPO NYARA ZA SERIKALI ZIKIMILIKIWA ISIVYO HALALI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA.

WILAYA YA MBEYA MJINI - AJALI YA GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 12.08.2012 MAJIRA YA SAA 16:00HRS HUKO ENEO LA ISENGO - PAMBOGO AIR-PORT JIJI NA MKOA WA MBEYA.

 GARI T.825 ABY AINA YA MITSUBISHI FUSO IKIENDESHWA NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO RONARD S/O LUGANO,MIAKA 5,KYUSA,MWANAFUNZI WA CHEKECHEA AIRPORT NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO . 

CHANZO NI MAREHEMU KUCHEZA BARABARANI NA WATOTO WENZAKE. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA KWA UCHUNGUZI NA GARI LIPO KITUONI. DEREVA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUWA MAKINI NA MAZINGIRA WANAYOCHEZA WATOTO WAO KWANI YANAWEZA KUHATARISHA MAISHA YAO PIA ANAMTAKA DEREVA HUYO KUJISALIMISHA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA ILI HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE.

WILAYA YA MBEYA MJINI - KUINGIA NCHINI BILA KIBALI.

MNAMO TAREHE 12.08.2012 MAJIRA YA SAA 18:00HRS HUKO UYOLE JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIMKAMATA IBRAHIM S/O ABDI,MIAKA 26,RAIA WA ETHIOPIA AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI . 

MTUHUMIWA YUPO MAHABUSU NA TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAENDELEA. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUJENGA TABIA YA KUTOA TAARIFA KWA MAMLAKA ZINAZOHUSIKA JUU YA WATU/MTU WASIYEMFAMU AU MGENI NA MAZINGIRA YAO WANAEMTILIA MASHAKA.

WILAYA YA MBEYA MJINI - KUPATIKANA NA BHANGI.

MNAMO TAREHE 12.08.2012 MAJIRA YA SAA 23:00HRS HUKO UYOLE SOKONI JIJI NA MKOA WA MBEYA. ASKARI POLISI WAKIWA DORIA WALIWAKAMATA FRANK S/O FELIX,MIAKA 20,MKINGA,MKULIMA MKAZI WA UYOLE NA NICODEM S/O ADAM,MIAKA 17,KYUSA,MKULIMA MKAZI UYOLE WAKIWA NA BHANGI GRAM 500 .  

MBINU ILIYOTUMIKA NI KUFICHA BHANGI HIYO KATIKA MFUKO WA RAMBO. WATUHUMIWA NI WAUZAJI NA WAVUTAJI WA BHANGI WAPO MAHABUSU. 

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA JAMII KUJIEPUSHA NA MATUMIZI YA MADAWA YA KULEVYA KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI


[ DIWANI ATHUMANI - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA

Post a Comment

Anonymous said... 14 August 2012 at 16:12

Safi sana
1.Itasaidia sana kupata kazi za uhakika, kama kweli wasanii wetu watakubaliana na ushauri watakao wanapewa na Watangazaji, MaDJ, Wadau, Wasikilizaji/Mashabiki na Producers....

2.Muziki imeonekana ni kazi ya kimbilio la vijana wengi waliopoteza mwelekeo wa maisha dats y umepoteza weledi katika jamii.

3. Baraza la Sanaa liweke vigezo sahihi vitavyotakiwa kwa mtu anayetaka kuingia katika tasnia hiyo kuvikidhi then asajiliwe..

 
Top