Menu
 

Soko la Samaki la Kasanga.
 Mazungumzo yakiendelea Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa. Kutoka kulia ni Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Rukwa Emmanuel Kachewa, Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Moshi Chang'a, Mrs. Katyega, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya, Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Alhaj Salum Mohammed Chima na Katibu Tawala Wilaya ya Kalambo Florence Mtepa.
 Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega Ofsini kwake jana alipotembelea Mkoani Rukwa kwa ajili ya kufuatilia miradi mbalimbali ya maendeleo ambapo alitembelea Soko la Samaki la Kasanga pamoja na kujionea maendeleo ya mradi wa umeme kwenda Wilaya ya Nkasi.

Hakika ziara ya Mkurugenzi huyo Msaidizi imekuwa ya mafanikio makubwa kwani baada ya kutembelea Soko kubwa la Samaki la Kasanga na kujionea umuhimu uliopo wa nishati ya umeme katika kuendesaha soko hilo ameahidi kupitia Shirika lake kuwa soko hilo litapatiwa Jenereta kubwa mbili kila moja ikiwa na uwezo wa 50KV. Alisema kuwa Umeme utakaozalishwa kutokana na Jenereta hizo utaweza pia kuhudumia Vijiji vya jirani vinavyolizunguka Soko hilo.
Jitihada za kulipatia Soko hilo umeme zimekuwa zikipewa msukumo mkubwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya ambae amekuwa akilifuatilia kwa karibu ambapo amefanikiwa kumpeleka kiongozi huyo wa Tanesco hadi eneo la mradi huo ikiwa ni katika jitihada zake za kutekeleza agizo la Mhe. Makamu wa Rais alipofanya ziara yake Mkoani Rukwa na kutoa agizo kwa uongozi wa Mkoa ushirikiane na Tanesco kuhakikisha Soko hilo linapatiwa umeme.
Akiwa Mkoani hapa Kiongozi huyo wa Tanesco alikuta baadhi ya mapungufu katika utekelezaji wa mradi utakaopeleka umeme Wilayani Nkasi ambapo walishauriana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ambapo walikubaliana litafutwe suluhu la changamoto hizo badala ya kulaumiana ili kukamilisha mradi
huo muhimu kwa Wilaya ya Nkasi na Mkoa wa Rukwa kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya akizungumza na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi  Uwekezaji wa Shirika la Umeme Nchini TANESCO Maneno Katyega (Kushoto) na Kaimu Meneja wa Shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Rukwa Emmanuel Kachewa walipotembelea Soko la Samaki la Kasanga jana.Picha na Habari na Afisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa-Hamza Temba

Post a Comment

 
Top