Menu
 

Tamasha la Tanzanite Sports Festival litaanza kutimua vumbi Agosti 22 mwaka huu katika Uwanja wa Tandale Mji mdogo wa Tukuyu,Wilayani ya Rungwe Mkoani Mbeya.

Akizungumza kupitia Kipindi cha Sports Bomba kupitia Kituo cha redio Bomba FM kinachorusha masafa yake kupitia mawimbi ya 104.0,Mratibu wa tamasha hilo Magige Flavian,amevitaja vituo mbalimbali ambavyo vitashiriki tamasha hilo kuwa ni Morogoro Youth Academy kutoka Mkoa wa Morogo, Zamaleki Sports Academy kutoka Mkoa wa Njombe na Mbeya Sports Centre(MBASPO).

Vingine ni Forest Youth Soccer Aspirants(Four ISSA),Majeshi Kids Soccer Academy kutoka Mkoani Dar es salaam na Tukuyu Sports Centre ya Wilaya ya Rungwe mkoani hapa.

Ameongeza tamasha hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo riadha,mpira wa pete,mpira wa miguu na michezo mingineyo mingi na vikundi mbali mbali vya ngoma na wasanii mbalimbali watashiriki katika tamasha hilo.

Hata hivyo Mratibu huyo Magige amesema lengo la tamasha hilo la Tanzanite Sports Festival ni kukuza vipaji na kuchangia ujenzi wa Kituo cha Rungwe.


Post a Comment

 
Top