Menu
 


Viongozi na wanachama wa tawi la CHADEMA London katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa Tawi lao.
---
Siku ya Jumanne  tarehe 7 August 2012, tawi la CHADEMA London lilizinduliwa rasmi. Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa kamnda Godbless Lema ambaye pia alijitolea kuwa mlezi wa tawi hilo. 

Pamoja na uzinduzi huo uchaguzi wa viongozi mpito ulifanyika na wanachama wapya walijitokeza na kujiandikisha.

Kwa habari zaidi zihusianzo na tawi la CHADEMA London wasiliana na Katibu Mwenezi Kamanda Chris Chagula au Mwenyekiti wa tawi Kamanda Chris Lukosi.
Kamanda Godbless Lema akiongea machache wakati wa uzinduzi wa tawi la CHADEMA jijini London nchini UK. Katika mambo aliyo yaongea ni pamoja na kujitoela kuwa mlezi wa twai la London na kwa kuanzia alikabidhii pesa taslimu dola za kimarekani 200 kwaajili ya kusaidia shughuli za chama.
Mwenyekiti wa tawi la CHADEMA London kamanda Chris Lukosi akimwaga sera zake wakati wa uzinduzi huo.
 Kamanda Dr. Alex ambaye ni mweka hazina akimwaga sera zake.


Mwenyekiti wa CHADEMA London kamanda Chris Lukosi akimtambulisha bwana Magabe ambaye ndo moja wapo wa watu walio wezesha tawi la CHADEMA kufunguliwa nchini UK.
 Makamu mwenyekiti Liberatus akichukua minutes.
 Katibu wa vijana Emmanuel Lunyama akimwaga sera.

 Mwenyekiti akionyesha uzalendo wa chama chake.
 Jessica Maduhu Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake  CHADEMA tawi la London akimwaga sera zake na kushukuru kwa kuchaguliwa.
 Magareth katibu wa Baraza la wanawake la CHADEMA tawi la London akiongea machache.

Post a Comment

 
Top