Menu
 
Vifaa mbali mbali vinavyouzwa kwa jumla na rejareja 

Kwa wale ambao wenye moyo wa kutoa na kusaidia jamii husika zenye matatizo nchini Tanzania.

Kuna University of washington surplus iliopo jijini Washington Seattle huwa kuna vifaa mbali mbali vya teknolojia, vinauzwa kwa bei rahisi, kupikwa minaada, kama vifaa vya shule mahospitalini n.k

Na kama tutakuwa pamoja kutojali idikati zetu na kuwa kijamii hapa ughaibuni nahisi kusaidia na kuondoa umasikini katika nchi yetu tutaweza hii ni njia moja wapo ya uzalendo wa kusaidia wasiojiweza na si chengine.

Tusitegemee kuomba misaada bali wenyewe tunaweza tukiwa na mioyo ya kutoa na kukubali kukusanya michango tukiwa na imani umoja na upendo kwa mwenye kutaka maendeleo ya nchi yetu kwa jumla, kwa kuwafikiria dungu zetu wenye matatizo nyumbani, kwani Jamii iliyostaarabika ni yenye kuheshimu Mawazo na Mitazamo ya wengine ili kujijenga na kusaidia wengine.

Mchango wako katika kazi yoyote ulenga kujenga nchi yetu kwa mwenye uchungu wakutambua shida na mitazamo ya kusaidia wengine kama walivyokuwa wakifanya nchi jirani ni mfano mzuri wa kuigwa ili nasisi tuonekane wana Diaspora tunaojali maendeleo ya nchi yetu kwa jumla, kwani maendeleo ya nchi huletwa na wananchi wenyewe na sio wageni wala kuitegemea serekali.
Bofya hapa kwa taarifa zaidiSwahilivilla Blog.

Post a Comment

 
Top