Menu
 

Na Ester Macha,Ileje.
Serikali wilayani Ileje Mkoani Mbeya imesema kuwa baada ya kuwepo kwa malalamiko ya kutokamilika kwa miradi ya sekta ya afya inayoelekezwa na fedha zinazotolewa na Serikali sasa miradi hiyo kusimamiwa na wananchi wenyewe na kufuatilia  matumizi sahihi ya fedha za umma.

Kauli hiyo ilitolewa wiki iliyopita na Mkuu wa Wilaya ya Ileje Bi.Rosemary Senyamule wakati akizindua mradi utakaowashirikisha wananchi na kuwajengea uwezo ili waweze kuwajibika katika miradi yao katika maeneo yao na kufuatilia matumizi sahihi ya fedha zinazotolewa kwa ajili ya miradi hiyo.


Alisema kuwa mradi huo unadhadhiliwa na(FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY)ambao utaweza kusaidia miradi mingi ya sekta ya afya ambayo imekuwa ikilalamikiwa na wananchi kutokana na kutokamilika kwa wakati na matumizi yake kutokuwa sahihi na hivyo wananchi kuzua maswali mengi.


Akizungumza wakati  wa uzinduzi huo Mkurugenzi wa Shirika la Hossan Ows Center Bw.Nsanya Mwalyego alisema  kuwa katika ripoti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya sekta ya afya  wilayani Ileje iliyotolewa na Idara ya afya kwa mwaka 2010/2011  inaonesha miradi mingi wilayani humo imeshindwa kukamilika licha ya  serikali kuu kuelekeza fedha katika miradi hiyo.


Alisema kuwa baadhi ya wananchi ambao ndio walengwa wa kuletewa miradi na serikali  wameonesha kutokuwa wawajibikaji katika miradi yao na hivyo kusababisha kuwa hafifu licha ya kuwa wanatakiwa kuwajibika katika miradi yao ya maendeleo ambayo imeletwa kwa ajili ya kusaidia wananchi.


Mmoja wa wananchi wa Wilaya ya Ileje Bw. Kasele Msongole alisema kuwa kuanzia sasa watakuwa mstari wa mbele katika kusimamia miradi ya afya ambayo inatolewa na serikali,mara nyingi fedha za miradi zimekuwa zikishindwa kufanya kama ilivyolengwa kutokana na walengwa wenyewe kutokuwa makini na miradi yao.


Hata hivyo Mkuu wa Wilaya hiyo amewapa jukumu wananchi la kuimarisha mradi wa kuimarisha uwajibikaji wa jamii ya Ileje katika  kusimamia mipango ya maendeleo ya sekta ya afya.

Post a Comment

 
Top